Tuesday 28th, January 2025
@Halmashauri ya Msalala
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala anawatangazia wananchi wote kuwa tarehe13/08/2024 mwenge wa Uhuru tutaupokea katika Halmashauri yetu.Hivyo wananchi wote tujiandae kuupokea mwenge wetu wa Uhuru na kuutendea Haki. Tutaupokea mwenge wa Uhuru katika kata ya Bulige ukitokea wilaya ya Shinyanga Vijijini, mwenge utakeshaSegese na baadae tutaukabidhi Halmashauri ya Ushetu. Wananchi wote tujitokeze kwa wingi kuutendea haki mwenge wa Uhuru.
Imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Msalala.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.