Tuesday 28th, January 2025
@Bugarama
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala anawatangazia wananchi wote kuwa tarehe 01/07/2018 kutakuwa na Uzinduzi wa Gulio na Mnada katika stendi ya mabasi iliyoko Bugarama. Kutakuwa na nyama choma, vinywaji vya aina mbalimbali, mazao, matunda na bidhaa tofauti tofauti. Wasanii wa musiki wa asili akiwemo mwana moto wa Mwanza na wengine wengi watatoa burudani katika sherehe hiyo. Usiombe kukosa.
Imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Msalala.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.