AFISA ELIMU MKOA ATETA NA WALIMU
Afisa elimu Mkoa wa shinyanga awaasa na kuwakumbusha walimu kutimiza majukumu yao katika mazingira
yao ya kazi haya yamezungumzwa leo na Afisa Elimu huyo Ndg. Mohamed Kahundi katia kikao kilichofanyika
leo tarehe 14/03/2018 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala ambapo kikao hicho
kilihudhuriwa na Afisa taaruma Mkoa, Walimu wakuu wote wa shule za Msingi na Sekondari, Waratibu Elimu
Kata , Aafisa elimu Msingi na Sekondari pamoja na mzibiti ubora wa shule Wilaya.
Afisa elimu Mkoa aliwataka wadau hao wa elimu kushirikiana kwa pamoja kuimalisha usimamizi wa shule
ilikuweza kuinua taaluma ya Elimu ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla, pia Afisa elimu aliwaagiza
wakuu wa shule kutokuhamisha wanafunzi kiholela waliokatika Madarasa ya mtihani na badarayake utaratibu
ufuatwe wa uhamishaji wanafunzi kwa njia ya mfumo wa Prem. Smbamba na hilo Afsia elimu alitilia mkazo
uboreshaji na usimamizi wa mazingira ya shule ikiwa ni sambamba na upandaji miti kwa kila mwanafunzi
kama agizo la mkuu wa mkoa linavyo agiza.
Nae afisa taaruma mkoa Ndg. James Malima aliwakumbusha walimu hao kufanya kazi kwa kuzingatia maadili
na miiko ya utumishi wa umma, Sambamba na hilo Afisa taaluma huyo aliwataka walimu wakuu kuwasimamia
walimu walio chini yao kwa ukaribu zaidi kwani hii itawafanya Walimu kutekeleza majukumu yao vizuri ikiwa ni
pamoja na ufundishaji mzuri ndani na nje ya darasa. Pia aliwaagiza walimu wote wa Elimu Sekondari na Msingi
kuwasimamia wanafunzi katika ushiriki wa michezo mashuleni kwa shule za umma na za binafsi kwani
michezo ni ajira na nihaki ya msingi kwa watoto.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.