AMREF YATOA MWANGA KWA VIJANA MSALALA
Kikao kilicho andaliwa na shirka la Amrefu katika ukumbi wa Vigmark Hotel Iliyoko Mkoani Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali toka Mkoani na viongozi toka Halmashauri ya Msalala ambao ndio wanufaika wa mradi huo. Katika kikao hicho mgeni rasimi alikuwa ni kaimu Mkuu wa Mkoa wa shinyanga Ndg. Albert Msovelo aliye ongozana na wataaram mbalimbali toka Mkoani pamoja na Meneja mradi Ndg. Sarafina Mkuwa
Katiaka kikao hicho Meneja Mradi Ndg. Sarafina Mkuwa alisema kuwa mradi wa Amrefu wanao uendesha katiaka Halmashauri ya Msalala unatarajiwa kuwafikia vijana 6041 kati yao wasichana ni 2967 na wavulana ni 3074 ambapo amesema kuwa mradi huo unalenga kuwasaidia watoto wa kike kupunguza mimba za utotoni au kumaliza taito hilo kabisa vijana hao wamepatiwa elimu ya Afya ya uzazi ambayo itawasaidia kujitambua na hivyo kupelekea kupungua kwa mimba za utotoni.
Pia alisema kuwa mradi huo umewajengea uwezo viongozi wa ngazi ya Mkoa, Wilaya, Kata na vijiji hii yote ni kwa lengo la kumsaidia mtoto wa kike ili aweze kutimiza ndoto zake .
Kaimu Mkuu wa Mkoa nae alieleza kuwa watu wote wanapaswa kutekeleza kwa umakini na kwa usahihi yale yote ambayo waendeshaji wa Mradi wanayatoa napia mradi huu unalengo la kumwelimisha kijana wa kike kwani ukosefu wa elimu na mira potofu ndiyo chanzo cha mimba za utotoni kwa mtoto wa kike pia mradi huu uwe chachu kwa wadau wengine kwani mradi huu utapunguza utoro kwa wanafunzi.
Pia makamo mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya masalala Ndg. Benedicto Manuari aliuomba uongozi wa Shirika la Amrefu kuonauwezekano wa kuongeza muda wa kutoa huduma kwa jamii kwani matokeo ni mazuri lakini muda unakuwa hautoshelezi.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.