Baraza la Madiwani lililoketi tarehe 16 hadi 17/11/2017 pamoja na mambo mengine limejadili nidhani ya watumishi na kufikia maamuzi ya kuwafuza kazi watumishi watatu(3) kwa makosa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kosa la utoro kazini. Na mmoja kati yao waliomba arudishwe kazini na apewe barua ya onyo.
Akizungumza mbele ya Baraza la Madiwani na Wakuu wa Idara mbalimbali Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Ndg Zabron Donge alithibitisha hayo na kudai kuwa watumishi hao wamefukuzwa kazi na mmoja kati yao ameamriwa kurudi kazi mara baada ya kukutwa na hatia na kuomba apewe barua ya onyo.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.