Mkurugenzi Mtendaji(W) Ndg.Khamis Jaafar katimba amewashukuru Wah.Madiwani kwa ushirikiano mzuri waliouonyesha katika mwaka wa fedha 2022-23
na kuiwezesha Halmashauri kupata Hati safi ambapo Halmashauri ilikusanya Jumla ya Tshs. 5,538,601.00 sawa na 103% ya kukusanya Tshs. 5,368,800,000.
Malengo haya yamefikiwa kutokana na ushirikiano mzuri uliopo kati ya wataalamu na viongozi mbalimbali ndani ya Halmashauri wakiwemo waheshimiwa
Madiwani na kuomba ushirikiano huo uendelee.
NDG. Katimba amesema katika mwaka huu wa fedha Halmashauri imejipanga kukusanya zaidi kwa kuwa yeye tayari amefanya vikao na wataalamu wote
ngazi ya kijiji,Kata na Halmashauri na kutoa maelekezo mbalimbali huku msisitizo ukiwa ni kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato na kuwaomba Waheshimiwa
Madiwani na Wananchi wote wa Msalala kumuunga mkono katika Jitihada hizo.
Aidha Mkurugenzi huyo amewaomba wananchi wa halmashauri na Watanzania kwa ujumla kuchangamkia fursa za uwekezaji ndani ya Halmashauri
ikiwemo ununuzi wa viwanja katika maeneo ya kata za Isaka, Segese, Kakola na Bulige kwani ni maeneo ya kimkakati kwa kuwa yamepimwa na yana huduma
muhimu kama Maji toka ziwa viktoria,Umeme,Vituo vya Afya, barabara zinazopitika mda wote kwenda Mwanza na Geita. Uchumi wa halmashauri unategemea
madini ya dhahabu ambapo kuna mgodi mkubwa wa Barrick Bulyanhulu na machimbo ya wachimbaji wadogo wadogo ambao wanachajia mapato kwa 75%,Mifugo
Kilimo cha zao na mazao kama Mpunga,dengu,na biashara ndogondogo zinachangia 25%
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Mibako Mabubu amepongeza jitihada zinazofanywa na Halmashauri inayoongozwa na Ndg.Khamis J. Katimba
kwani ndani ya Mda mfupi alioutumikia ndani ya Halmashauri, Mabadiliko yameanza kuonekana na kuahidi kwa niaba ya waheshimiwa Madiwani wote
kutoa Ushirikiano lengo ni kuwezesha Halmashauri kukusanya mapato ili kuwezesha miradi katika kata mbalimbali kutekelezwa kwa wakati.
Katika Kikao hicho Uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ulifanyika ambapo Diwani wa Kata ya Mwalugulu Mhe. Frola Sagasaga
mgombea kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) amefanikiwa kutetea kiti chake kwa kupata kura zote 22 za ndio. Pia Mwenyekiti wa Halmashauri
amefanya mabadiliko madogo kwenye kamati za Madiwani za Halmashauri.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.