Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Msalala limempongeza Mkurugenzi Mtendaji (W) na wataalamu wake kwa kuandaa ripoti nzuri ya ufungaji wa mahesabu kwa mwaka 2021/22. Pongezi hizi zimetolewa na makamu mwenyekiti wa Baraza hilo Mhe. Frola sagasaga wakati wa kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2021/22 Halmashauri ya Msalala ilikusanya jumla ya Tshs. 4,870,155,132.41 sawa na asilimia 96 ya makisio ya mwaka TSh 5,086,860,800.00, kutoka vyanzo mbalimbali, fedha za ruzuku ni Tshs. 821,977,211.91 ambazo ni fedha za kufidia mapato ya ndani kutoka serikali kuu na OC proper huku Fedha za mishahara zikiwa ni Tsh. 15,950,940,457 na T Shs. 9,841,462,003.91 zimepokelewa kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo. Hadi kufikia Juni 30,2022 Halmashauri hiyo imetumia Tshs. 28, 552,439,760.97.
Taarifa hii imezingatia mfumo wa ufungaji wa hesabu za kimataifa ujulikanao kama IPSAS, ambapo Wah. Madiwani wamemtaka Mkurugenzi (W) kuhakikisha madeni yanayodaiwa yanakusanywa kwa wakati ili kuepusha Halmashauri kuwa na hoja za ukaguzi sambamba na kuweka utaratibu mzuri wa kuwalipa wazabuni kwani madeni hushusha hadhi ya Taasisi.
Taarifa hii imeandaliwa na kutolewa na kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.