Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kahama mkoa wa Shinyanga kimeridhishwa na shughuli za maendeleo zinazofanywa na Halmashauri ya Msalala kupitia wataalamu mbalimbali kutoka ngazi ya kijiji,kata na Halmashauri
kwani fedha nyingi zinazoletwa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzani Dr.Samia Hassain Suluhu,zinatendewa haki kwa kukamilisha miradi iliyokusudiwa kwa viwango
vya hali ya juu.Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kahama Mhe.Thomas myonga wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kilichoketi 30.10.2023 kujadili taarifa za shughuli za
utekelezaji za Halmashauri kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2023-24,mwenyekiti huyo amewapongeza Waheshimiwa Madiwani kwa kusimamia vema miradi ya maendeleo katika maeneo yao na hivyo kutekeleza ilani
ya CCM kwa vitendo. Mhe,Myonga pia amewapongeza viongozi wa vyama rafiki ndani ya Wilaya ya Kahama kwa kushirikiana na chama Tawala katika kupanga,kushauri na kukubaliana kwenye mambo ya msingi yanayohusu
maendeleo ya wanakahama,Shinyanga na Tanzania kwa ujumla kwani Rais wetu anafanya maendeleo kwa Watanzania wote na sisi kama wanasiasa tunajukumu la kuungana kwa pamoja na tufanye siasa za maendeleo kwani
mwisho wa siku tunahitaji maendeleo kwa taifa letu.
Awali akifungua kikao hicho,mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala Mhe,Mibako Mabubu ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dr.Samia Hassain Suluhu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa
kuona umuhimu wa wananchi wa Halmashauri ya Msalala kuwa na jengo lao la Utawala kwa kutoa fedha na kuwezesha jengo la Halmashauri hiyo kukamilika na kuanza kutumika,sisi kama viongozi wa Halmashauri
tunaahidi kutekeleza miradi yote iliyoletewa fedha kwa viwango vya juu na kwa wakati ili wananchi wanufaike kwa wakati na matunda ya Mhe.Rais wetu Dr.Samia Suluhu,kwa kweli haijawahi kutokea tangu ndani
ya Halmashauri kupokea fedha nyingi kiasi hiki na kufanikisha kukamilisha miradi mingi yenye mabilioni ya fedha,tunashukuru sana Rais wetu na tunakuombea kwa Mungu afya njema ili uendelee kututumikia
wananchi kwani tuna imani kubwa sana na wewe.Hoja hii imeungwa mkono Waheshimiwa Madiwani wote wa baraza hilo,baadhi ya waliounga mkono hoja hii ni Mhe,Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri na diwani wa kata
ya Mwalugulu ambaye amesema,Dr.Samia Suluhu amewezesha ongezeko la wasomi na kutoa ajira kwa kuboresha elimu,nae diwani wa Kata ya Mega Mhe.Patrick Mazuri amempongeza Mhe.Rais Samia Suluhu kwa kuwezesha
kuwezesha umeme kufika vijijini na kuchochea maendeleo kwa haraka na Mhe.Joseph Manyara diwani wa kata ya Segese ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kutoa huduma bora za afya kwani upatikanaji wa
dawa katika Halmashauri ni mzuri hivyo kuhakikisha afya za wananchi zinalindwa na akaiomba Halmashauri kumpatia greda kwa ajiri ya kuchonga barabara za Segese ambapo gharama za Mafuta wananchi wa Segese
watachangia.
Baraza limejadili kwa kina taarifa za utekelezaji za kila kata na kuomba wataalamu wazipitie kwa utulivu na kutoa majibu ya changamoto zilizowasilishwa ikiwemo utoaji wa makadirio ya majenzi yasiyoendana
na uhalisia wa bei sokoni,wananchi waliofanya kazi na Tanesco(REA) kutokulipwa fedha zao kwa wakati na kuomba wataalamu wa Halmashauri kuiga mfano wa mkurugenzi Mtendaji(W) NDG.Khamis Katimba wa kutembelea
maeneo mbalimbali ndani ya Halmashauri, hii inamsaidia kuijua vizuri Halmashauri yake hivyo wakuu wa idara fuateni nyendo za kiongozi wetu.Hoja hii imetolewa na Mhe.shija Luyombwa diwani wa kata ya Bulyanhulu
ambapo amempongeza Mkurugenzi Mtendaji(W) na wajumbe wa Baraza la Madiwani kwa usimamizi wao madhubuti wa miradi na kuwezesha Halmashauri kuhamia kwenye jengo jipya hii yote imetokana na jitihada za Mhe.Rais
Samia Suluhu kwa kutoa fedha kuwezesha miradi viporo kukamilishwa na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.Diwani huyo amemshukuru pia Mbunge wa jimbo la Msalala Mhe.Alhaji Idd Kassim Idd kwa kuisemea vizuri Halmashauri
na kushawishi Bunge kupitisha bajeti za kutekeleza miradi ndani ya Halmashauri.Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji(W) NDG.Khamis Katimba amepokea shukrani zilizotolewa na kuongeza kusema Halmashauri ipo kwa ajili
ya kuwatumikia wananchi hivyo wakati wowote yupo tayari kutumika na kuwaomba Madiwani hao kushirikishana uzoefu wa changamoto wanazokutana nazo katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku kwa kuwa changamoto
hutofautiana kulingana na mazingira yao ya kiutawala,Halmashauri ndani ya mwezi ujao itaanza maandalizi ya mpango na bajeti kwa mwaka ujao hivyo vipaumbele vya kila kata vitazingatiwa kwakuwa tayari mwongozo
upo kupitia sensa ya watu na makazi iliyofanyika 2022.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.