Halmashauri ya Wilaya ya Msalala imeamua rasimi kuhamia katika eneo lake la utawara lililopo katika kata ya ntobo Wilaya ya Msalala penye umbali wa takribani kilometa 25 toka Kahama Mjini kuanzia tarehe 28 ya mwezi Mai 2018 ambapo wakuu wote wa idara na vitengo wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndg. Simon Berege na kuitikiwa na watendaji wote wa ofisi kuu na hivyo siki hiyo walianza kufunga mizigo na kupakia kwenye gari maarumu ambalo lilitumika kusafirishia mizigo.
Sambamba na hilo Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Saimon Berege aliwaondoa wasiwasi watumishi wake na kuwaeleza kuwa mahari wanapokwenda ni nyumbani, na pia kunafulsa nyingi za uwekezaji kwani kuna maeneo makubwa yenye rutuba ambayo yanafaa kwa kilimo na ufugaji.
Kuanzia tarehe 28/05/2018 siku ya jumatatu ofisi zote na huduma zote zitatolewa katika eneo la ntobo.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.