HALMASHAURI YA MSALALA YAADHIMISHA SIKU YA UKIMWI DUNIANI
Halmashauri ya Msalala yaadhimisha siku ya UKIMWI Duniaaki katiaka kata ya Segese na kuhudhuriwa na Makamo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala Mh. Benedict Manuary ,Viongozi mabalimbali toka Halmashauri ya Msalala ,Wananchi toka maeneo mbalimbali kuzunguka Kata ya Segese pamoja na wawakilishi toka mashirika ya afya ya AGAPAH,AMREF NA SHIDEFA wakiongozwa na mkurugenzi toka shilika la SHIDEFA .
Aidha maadhimisho hayo yalienda sambamba na uhamasishaji wa kampeni ya upimaji VVU, Tohara kwa vijana wa kiume kuanzia miaka 10 na kuendelea mpaka miaka 100 pamoja na upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi kwa akina mama.
Akizungumza mbele ya mgeni rasimi Mratibu wa UKIMWI(w) Msalala Ndg Jackson Oswago alisema kuwa hali ya maambukizi ya VVU yamepungua kutoka asilimia 06% mwaka 2013 na kufikia asilimia 03% mwaka 2017 hivyo maambukizi hayo yamepungua kwa kiasi kikubwa sana na pia aliwaasa wananchi kujitokeza kwa wingi ili wapime afya zao.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.