HALMASHAURI YA MSALALA YAWA KINARA KWA MBIO ZA MWENGE 2017
Halmashauri ya wilaya ya Msalala iliyopo wilayani Kahama Mkoani Shinyanga imeibuka mshindi wa kwanza katika mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2017 kanda ya pili kanda hii inahusisha Mikoa ya Morogoro,Tabora,Simiyu,Shinyanga,Tanga,Iringa na Njombe. Wakati huohuo ikishika nafasi ya tatu Kitaifa. Hii ilitolewa jana katika maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambalage Nyerere ambapo pia ilikuwa ni siku ya kuzima mwenge wa uhuru . mwenge wa uhuru ukiwa wilayani kahama katika Halmashauri ya Msalala miradi nane(8) ulizinduliwa ,kuwekewa jiwe la misingi na kuonwa. Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama walihamasika kwa wingi kuulaki mwenge wa uhuru .
Mwiongoni mwa sababu za mafanikio haya ni pamoja na viongozi shupavu wa kamati ya ulinzi na usalama ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mh. Fadhir Nkurlu, ukaguzi na usimamizi wa mara kwa mara wa miradi ya shughuri za wananchi iliyofanywa na timu ya Menejimenti ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Bw. Simon Berege pia ushirikiano mzuri uliopo baina ya wananchi wa Msalala na wafanyakazi wa Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.