HALMASHAURI YA WILAYA YA MSALALA KWA KUSHIRIKIANA NA ACACIA YASAINI MKATABA WA UJENZI WA MAJENGO YA KITUO CHA AFYA .
Halmashauri ya wilaya ya Msalala yafanya makubaliano na kutiliana saini na kampuni ya uchimbaji madini ya ACACIA pamoja na wakandarasi kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya cha Bugarama kwa awamu ya pili inayo fadhiriwa na kampuni la uchimbaji madini la ACACIA. akizungumza hayo mbele ya wageni mbalimbali na waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala Ndg. Zabron Donge amesema kuwa kwakuhakikisha zoezi la ujenzi wa mradi huo linakwenda vizuri Halmashauri imechangia kia si cha Tsh.milioni sabini na tano (million 75) ili kufanikisha ukamilishwaji wa majengo hayo. Pia kaimu mkurugenzi aliwataka wakandarasi kuwatumia wanajamii wanao zunguka eneo husika ilikujipatia kipato mbalimbali pamoja na kuwataka makandarasi waliopatiwa tenda hiyo endapo kunakitu chochote kitakacho tokea nje ya utaratibu waliokubaliana taarifa ipelekwe kwa Mkurugenzi mara moja kwani lengo la ujenzi wa majengo hayo ni kutaka kufikisha huduma kwa jamii ya watanzani.
Pia Kaimu Meneja wa mgodi wa ACACIA alisema kuwa mradi wa kwanza ulighalimu kiasi cha dola za kimareka laki nne na themanini na tano elfu ambazo ni sawa na Tsh. Bilioni Mmoja Milioni miatisa na milioni tisini ambapo wanatarajia kutumia kiasi cha dora za kimarekani laki tano ambapo ni sawa na Tsh. Biliono Moja Milioni mia moja themanini na tisa laki sita na sitini na moja elfu miamoja therasini ma mija ambapo kwa jumla mradi wote utagalimu kiasi cha zaidi ya pesa Kitanzania Bilioni Mbili na pia kuwataka wakandarasi kulipa service levy kwa Halmashauri na kuwa wazarendo kwa kuwatumia wakazi wa maeneo husika hasa kwa kazi za Kitanzanivibalua.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.