Halmashauri ya Wilaya yaMsalala imeomba idhini ya kufanya manunuzi ya vifaa tiba na madawa yaZaidi ya milioni ishirini na tano, ambapo Mkurugenzi mtendaji (W)ndugu Simon Berege aliwasilisha ombi hilo mbele ya baraza la Madiwanileo katika kikao cha baraza la madiwani katika ukumbi wa Halmashaurihiyo uliopo katika kata ya Ntobo. Akiwasilisha ombi hilo ndg. SimonBerege amesema “ vituo vyetu vya kutolea huduma vingi vimeboreshahuduma kupitia fedha za RBF, bima za jamii, fedha za papo kwa papo nahivyo Halmashauri ikiwa mmiliki wa vituo hivyo imeona ni vemaiviongezee fedha kwa ajili ya kununulia madawa ambayo yatatumikakuhudumia jamii.
Wakichangia hoja katika ajendahii, waheshimiwa madiwani wameipitisha bajeti hii na kuitakaHalmashauri kuongeza fedha hizo katika bajeti ya kipindi kijacho ilikuwezesha vituo hivyo kuwa na madawa na vifaa tiba muda wote nakuondoa au kupunguza tatizo la ukosefu wa madawa na vifaa tiba ndaniya Halmashauri. Waheshimiwa madiwani hao wamemtaka MkurugenziMtendaji (W) kusimamia madawa na vifaa tiba hivyo pindivitakaponunuliwa kwani kuna baadhi ya watendaji wa Halmashauri siowaaminifu.
Katikakikao hicho mada mbalimbali zimejadiliwa na kutolewa ufafanuzi naufumbuzi, miongoni mwa mada hizo ni fedha zinazopatikana kutokana nauendeshaji wa shughuli za madini katika mgodi wa Bulyanhulu ambapoMkurugenzi Mtendaji amesema hadi kufikia leo mwekezaji alikuwahajalipa fedha zinazorudi kwa ajili ya kutekeleza miradi ya jamii,(fedha za CSR) ambapo Mkurugenzi huyo amesema wameishauri fedha hizozilipwe Halmashauri ili kuweza kukamilisha mradi mmoja utakaoonekanabadala ya kulipa vijiji kidogo kidogo, waheshimiwa madiwani wamemtakamkurugenzi Mtendaji kumwaandikia barua mwekezaji ili alipe fedhandani ya siku saba vinginevyo baadhi ya waheshimiwa Madiwaniwatakwenda kuomba msaada TAMISEMI ili kuwezesha miradi kukamilika kwawakati kwani ikumbukwe kuna suala la madarasa kwa wanafunzi wasekondari yanahitaji kukamilika.
Imetolewana kitengo cha Habari na Mawasiliano Halmashauri ya Msalala.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.