Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
inayoongozwa na MHE. Joseph Manyara imeitaka Halmashauri hiyo inayoongozwa
na NDG. Hamis Katimba Mkurugenzi Mtendaji(W) kuhakikisha miradi inayotekelezwa
ndani ya Halmashauri kukamilishwa kwa wakati na kwa viwango vya ubora.
Kauli hii imetolewa wakati wa kikao cha kamati hiyo ambayo imetembelea miradi
4 ambayo inajengwa kupitia fedha za mapato ya ndani yenye thamani ya Tsh. 287,000,000
katika kata za segese, Bulyanhulu,Mega na Bulige ambazo zitanufaisha wananchi katika
nyanja za Biashara na Uwekezaji, Kilimo na Mifugo na Usimamizi wa Mazingira na Maliasili
ambapo Jumla ya Tsh. 7,920,000 zinatoka Serikali kuu na Kufanya fedha zilizotumika katika
robo ya nne kuwa Tsh. 294,920,000.
Awali akimkaribisha Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mkurugenzi Mtendaji (W) NDG. Hamis Katimba
amesema Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira ni muhimu katika kuleta maendeleo ya uchumi wa mtu
mmoja mmoj, Kikundi, Halmashauri na Taifa kwa ujumla. Kamati hii ina mchango mkubwa kwa ustawi
wa wanamsalala hivyo wajumbe wana haki ya kutoa elimu ya miradi mbalimbali inayofanywa na Serikali
ya Awamu ya sita inayoongozwa na MHE. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Hassain
Suluhu.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Halmashauri ya Msalala.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.