KITUO CHA AFYA NGAYA CHAMELEMETA
Leo tarehe 12/10/2018 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ndg. Simoni Berege amefanya ziara katika zahanati ya Ngaya iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Msalala na kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Mama na mtoto, upasuaji, Maabara pamoja na Jengo la kuhifadhia Maiti. Ambapo alikuta ujenzi wa majengo hayo unaendelea vizuri na mpaka sasa wamekwisha maliza ujenzi wa Misingi na wapo kwenye maandalizi ya umwagaji wa jamvi.
Akifanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa majengo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Ndg. Simoni Berege alitowa wito kwa wakandarasi hao kufanya kazi zao kwa weredi wa hali ya juu napia kwa kasi ya kutosha ili majengo hayo yaishe kwa muda uliopangwa, pia Mkurugenzi huyo alizungumza na kamati zote zinazo simamia mradi huo na kuzitaka ziwe na ushirikiano kwani kwa kushilikiana pamoja kunaleta mafanikio mazuri na yenye tija .
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.