Katika awamu hii ya serikali ya awamu ya tano Halmashauri nchini zilitakiwa kuwa wabunifu katika kuhakikisha miradi ya Halmashauri inatekelezwa kupitia bajeti ya serikali kuu, Halmashauri na wadau mbalimbali ambapo pia Halmashauri zilitakiwa kujikita katika kuandika maandiko na kuyapeleka serikali kuu na kwa wadau mbalimbali.
Kwa kipindi cha robo ya pili Halmashauri ya Msalala ilifanikiwa kuandika na kupeleka maandiko sehemu mbalimbali ambapo pia Halmashauri ilifanikiwa kupata fedha nyingi toka Serikali kuu kupitia maandiko hayo, mifano ya fedha hizo ni fedha za uwezeshaji upimaji wa viwanja vya ardhi zilizotolewa na wizara ya ardhi na makazi, fedha za mradi wa maji toka ziwa viktoria wa kakola Ilogi, mradi wa ujenzi wa shule na ukarabati wake. Hii ni baadhi tu ya mifano ambayo imekamilishwa kupitia fedha zilizotolewa na Serikali kuu.
Ipo miradi iliyokamilishwa kupitia maandiko kwa wadau mbalimbali ikiwemo ujenzi wa maghala 2 ya kuhifadhia mazao yaliyojengwa na CABUIPA katika kata za Bugarama na Shilela. Ujenzi wa shule za sekondari za Mwakata, Mega na Kashishi ambapo wadau mbalimbali wakishirikiana na Halmashauri wameshiriki kukamilisha shughuli hizi.
Maneno hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala ndugu Simon Berege katika kikao cha baraza la Madiwani cha robo ya pili kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo uliopo katika kata ya Ntobo.
Imetolewa na kitengo cha mawasiliano serikalini,
Halmashauri ya Msalala.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.