“MALIZENI UJENZI KWA WAKATI’’
Ziara ya madiwani na wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala iliyofanyika jana tarehe 23 na 24 aprili,2021 katika maeneo mbalimbali yenye miradi ikiwemo mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya inayojengwa katika eneo la Kata ya Ntobo. Katika ukaguzi huo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Mh. Mibako Mabubu aliwataka local fundi wote walio pewa tenda ya ujenzi wa majengo yote ya Hospitali hiyo kukamilka kwa ujenzi huo mapema kabla ya mwaka wa fedha kuisha ili kuepuka fedha kurudishwa. Aidha kamati hyo iliwaagiza wasimamizi wa ujenzi huo kuongeza vifaa pamoja na vibaruwa ili kuongeza kasi ya ujenzi wa majengo hayo
Pia madiwani walikaguwa ujenzi wa jengo la Makao makuu ya Halmashauri na kukuta ujenzi ukiendeleana upo kwenye hatua mbalimbali. Kamati hiyo iliwataka mafundi hao kuongeza kasi ya ujenzi ili kuhakikisha jengo hilo linakamilika mapema kabla ya juni 30,2021.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.