MKUU WA MKOA SHINYANGA AWATAKA WAFANYAKAZI KUSHIRIKIANA NA WAH. MADIWANI
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga amewataka Waheshimiwa madiwani na Wataalamu wa Halmashauri ya Msalala kufanya kazi kwa pamoja ilikuweza kutatua matatizo mbalimbali ya wananchi kwalengo la kuleta maendeleo kwa Tanzania kwa Ujumla. Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa katika kikao cha baraza la Madiwani la Halmashauri ya Msalala lililokuwa likipitia majibu ya Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali lililofanyika tarehe 26/05/2017 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Aliwataka Wataalamu wa Idara mbalimbali pamoja na Vitengo kushirikia na katika kuhakikisha hoja zaukaguzi zinapatiwa majibu na hoja hizo kufungwa kwani hapendi kuona Halmashauri yeyote katika mkoa wa Shinyanga ikiendelea kuwa na hoja pasipo sababu. Aliwaomba Wakaguzi wa mkoa wazitembelee Halmashauri ilikuweza kukagua miradi iliyokuwa imehojiwa kwa kuwa miradi hiyo tayari imekamilika na inafanyakazi.
Sambamba na hayo Mkuu wa Mkoa aliwataka waheshimiwa madiwani kufanya kazi kwaumoja na kuepuka kuwa na mivutano ambayo hainatija kwani kufanyahivyo nikurudisha nyuma maendeleo ya wananchi wa Msalala. Alisisitiza kutumia uwiano mzuri wa uanzishaji wa miradi ndani ya Halmashauri ilikuhakikisha kila kata inafaidika kutokana na miradi hiyo, kwani lengo kuu la serikali ni kuhakikisha wananchi anapata huduma bora katika Nyanja mbalimbali ikiwemo Maji, Elimu, Afya na Kilimo. Aliwaomba waheshimiwa madiwani na wataalamu kuhakikisha wanawahamasisha wadau mbalimbali wenye uwezo wakujenga viwanda wajenge pia alisema Shinyanga imejaliwa kuwa naardhi nzuri hivyo nivizuri wananchi wakapewa elimu juu ya kuanza mapema kilimo pindi msimu unapo anza.
Mkuu wa mkoa alikabidhi zawadi ya mashuka kwakituo cha afya cha Chela namabati kwashule za msingi nne zinazo patikana katika Halmashauri hiyo. Alimaliza Kikao kwakuwataka wataalamu nawaheshimiwa madiwani kuanzaujenzi wa Makao Makuu mara moja kwakuwa ramani yaujenzi wa makao makuu ilishakamilika natayari Mzabuni alishapatikana. Pia alimtaka Mwenyekiti wa Halmashauri kuangalia uwezekano wakupata sehemu ya kuweka majengo ya muda ya Ofisi ili kuwawezesha wafanyakazi wa Halmashauri ya Msalala kuhamia kwa lengo la kupeleka huduma karibu na wananchi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala Mhe. Mibako Mabubu alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwakuendesha kikao vizuri na kuahidi kutekeleza yote yaliyo zungumzwa katika kikao hicho nakuahidi kufanyakazi kwakujituma na kuwataka waheshimiwa Madiwani kusimamia shughuli zote zinazotekelezwa katika maeneo yao.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.