Kila ifikapo tarehe 08 ya mwezi wa 3 Dunia nzima huadhimisha siku ya wanawake Duniani. Sherehe
hiyoilihudhuriwa na wageni mbalimbali toka Halmashauri ya Msalala ,ikiwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake
Msalala Ndg Matrida Msaoma pamoja na wadau mbalimbali, Maadhimisho hayo yamefanyika katika Kata ya
Segese Wilayamni Msalala.
Katika maadhimisho hayo ya Siku ya Wanawake Duniani Halmashauri yaWilayani ya Msalala imetoa hundi
yenye thamani ya shilingi milioni saba kwa vikundi vitatu vya wanawake wajasirimali.
Akikabidhi hundi hiyo katika kata ya Segese yalikofanyika maadhimisho hayo kwa ngazi ya Halmashauri, Afisa
Maendeleo Jamii wa Halmashauri ya Msalala, Ndg, ALIADINA PETER amesema fedha hizo zitawasaidia
wanawake hao kujikwamua kiuchumi.
Kwa upande wao baadhi ya wanawake ambao wamepewa fedha hizo wameishukuru Halmashauri hiyo na
kuiomba iendelee kutoa elimu zaidi ili vikundi vingine vifaidike na fursa hiyo ya mikopo kwa akina mama.
Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake wa Halmashauri ya Msalala Ndg, MATRIDA MSOMA amesema siku
ya wanawake duniani ni muhimu kwao katika kumkomboa mwanamake dhidi ya mfumo dume na kandamizi zidi ya mwanamke pamoja Unyanyasaji
unaofanywa na baadhi ya Wanaume wasio waadirifu.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.