MWENGE WAPONGEZA MIRADI MSALALA
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Ndg. Charles Francis Kabeho ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Msalala kwakuwa na miradi yenye kukidhi vigezo vyote vya ubora na matumizi sahihi ya fedha zinazotolewa na serikali pamoja na wafadhili wengine.
Ndg. Charles Francis Kabeho amezungumza hayo leo katika viwanja vya makabidhiano ya mwenge katika viwanja vya Kagongwa kati ya Halmashauri ya Msalala na Halmashauri ya Mji Kahama ambapo alizungumza hayo mbele ya viongozi mbalilimbali wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Ndg. Anamringi Macha , Wananchi pamoja na Waandishi wa habariwaliohudhuria shamrashamra za makabidhiano hayo ambapo aliipongo Halmashauri ya Msalala kwa kufanya vizuri katika usimamizi wa miradi ya maendeleo ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala Ndg. Simon Berege. Sambamba na hilo kiongozi wa Mbio za Mwenge Ndg. Kabeho aliushukuru uongozi wa Halmashauri ya Msalala pamoja na Wananchi kwa kujitoa na kuutendea haki mwenge wa uhuru kwa mapokezi mazuri, kwani kilawalipo pita walikuta wananchi wengi wamejitokeza kuushangilia na kuupokea mwenge wa uhuru.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.