Sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani nchini Tanzania zimeadhimishwa kitaifa mkoani Kilimanjaro huku Mkoani Shinyanga zikiadhimishwa kimkoa katika kijiji cha Kakola kata ya Bulyanhulu
Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama ambapo mkuu wa Mkoa wa Shinyanga MHE.Anamringi Macha amekuwa mgeni Rasmi katika Sherehe hizo.Taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi zimeshiriki maadhimisho hayo
huku Kauli mbiu ya Mei Mosi ya mwaka 2024 ikiwa ni nyongeza ya Mishahara ni msingi Bora na kinga ya hali Ngumu ya Maisha.
MHE.Anamringi Macha amewataka Watumishi kuendelea kuchapa kazi kwa bidii na ari kubwa ili kuhakikisha tunainua vipato vya mtu binafsi,mkoa na Taifa kwa ujumla kwani kupitia jitihada za mwananchi mmoja mmoja
ndipo maendeleo ya nchi yetu yanaweza kufikiwa kwa urahisi na akatoa wito kwa wafanyakazi wanaofanya kazi kwa mazoea kuacha tabia hiyo kwani ni kukwamisha jitihada na malengo ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa
na MHE.Rais Samia Suluhu anayehitaji wananchi kuwezeshwa kiuchumi ili kuinua pato la nchi na ni wafanyakazi wa Tanzania tunategemewa kufanikisha hili hivyo tujitoe kwa moyo wote kuwatumikia wananchi wetu.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama MHE.Mboni Mhita ameyapongeza mashirika mbalimbali ya Umma na Binafsi,Halmashauri za Wilaya,Manispaa,Ofisi za wakuu wa Wilaya za mkoa wa Shinyanga, Wanahabari na wananchi wote walio
jitokeza kwenye sherehe za maadhimisho ya sikukuu za Wafanyakazi kwani sherehe hizi ni zetu,nimefurahi kuona umati mkubwa wa Watumishi na wananchi kutuunga mkono yote hii ni kukubaliana na mazuri yanayofanywa na Serikali yetu
ya awamu ya sita,sio siri yanayofanywa na MHE.Rais Samia Suluhu yanaonekana,naomba miradi yote iliyokamilika ndani ya Halmashauri tuitunze kwa kuwa ni mali yetu.
Nae MHE.Mbunge wa Jimbo la Msalala MHE.Alhaji Idd Kassimu Idd licha ya Vikao vya Bunge kuendelea amehudhuria Sherehe hizi na kuweka bayana Baadhi ya Miradi iliyotekelezwa na kukamilika na kuanza kutoa huduma kwa wananchi kuwa
ni Shule ya Msingi Bulyanhulu,Shule ya Sekondari Bushingwe,Kituo cha Afya Bugarama,Shule ya Sekondari ya Wasichana Bulyanhulu.Hii ni baadhi ya Miradi iliyotekelezwa na Serikali yetu inayoongozwa na MHE.Rais Samia Hasain Suluhu
kwa kweli Kwa niaba ya wananchi wa Halmashauri ya Msalala tunamshukuru sana kwa kutuletea mabilioni ya fedha kukamilisha miradi mingi ya maendeleo ndani ya Halmashauri ya Msalala,haijawahi kutokea kupokea fedha nyingi ndani ya
mda mfupi.Mda si mrefu barabara yetu ya Kakola Kahama nayo itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami hivyo Wafanyakazi tuone fahari kuwatumikia wananchi kwani MHE.Rais anahitaji wananchi tuwatumikie kwa ufasaha.
Nae Mwakilishi wa TUCTA Mkoa NDG.Ramadhani Pangara ametaja baadhi ya changamoto zinazowakabili Wafanyakazi Mkoani Shinyanga kuwa ni kuchelewa kulipwa mafao kwa Wastaafu,Kikokotoo kiangaliwe kwa upya kwani kinatuumiza Wafanyakazi, baadhi ya Waajiri
kutopeleka michango ya Wafanyakazi wao kwenye Mifuko ya hifadhi ya Jamii na kuomba Serikali kuyapatia ufumbuzi changamoto hizo. Akihutubia Wafanyakazi Mkuu wa Mkoa huyo ameahidi kuzipatia ufumbuzi mapema changamoto zilizowasilishwa kwani Serikali
yetu ni sikivu hasa katika suala la kikokotoo mana changamoto hii ni ya nchi nzima hivyo suluhisho litapatikana kwa bahati nzuri pia Wabunge wetu wameishaishauri Serikali kupitia vikao vya Bunge letu hivyo Wafanyakazi wenzangu tuwe na uvumilivu wakati
Serikali ikiendelea kulifanyia kazi.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.