Mhe. Iddy Kassimu Iddy amependekeza kuundwa kwa kikosi kazi katika maeneo yote ya kukusanyia mapato ya Halmashauri ili kuondoa mianya ya upotevu wa mapato ya Halmashauri. Timu hiyo iundwe kwa kujumuisha Wah. Madiwani na Wataalamu ili kurahisisha uboreshaji wa mapato hayo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji (W) ndg. Charles Edward Fussi amekubaliana na pendekezo hilo na kuongeza kusema katika mwaka wa fedha 2022/2023 Halmashauri imepanga kufanya utafiti wa mazao mbadala sanjari na uanzishaji wa skimu za Umwagiliziaji kwani Halmashauri ya Msalala ni kitovu cha uzalishaji wa zao la mpunga kwa kanda ya ziwa ambalo kwa sasa limeathirika kutokana na mvua kuwa hafifu hivyo uanzishaji wa skimu za umwagiliaji utawezesha kilimo hicho kufanyika muda wote.
Wakichangia hoja waheshimiwa madiwani wamesema uanzishaji wa skimu hizo utakuwa muarobaini kwa wakulima wa zao la mpunga ndani ya Halmashauri hiyo kwani mpunga unaolimwa ndani ya Halmashauri unachangia kwa zaidi ya 60% ya mpunga unaozalishwa kanda ya ziwa hivyo pato la wanamsalala litaongezeka kwa kiasi kikubwa, waheshimiwa madiwani wameomba pia Halmashauri kuhamasisha wawekezaji kuwekeza mashine za kisasa za kukoboresha mpunga maeneo yote ya uzalishaji huo.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Halmashauri ya Msalala
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.