WAKAZI WA CHELA WANEEMEKA
Kituo cha Afya chela kilichopo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Msalala chaendele na ujenzi wa Wodi ya Wanawake Thieter na Maabara. Ujenzi huo ambao unaendelea kwa kasi ya hali ya juu ukiwa chini ya usimamizi wa Halmashauri ya Msalala pamoja na Wananchi wa Vijiji vinavyo zunguka kituo hicho.
Mbali na kusogezewa huduma pia ujenzi huo umegeuka kuwa neema kubwa kwa wakazi wa maeneo hayo kwani vibarua na wafanyakazi wa ujenzi huo wanatoka ndani ya viunga vinavyo zunguka eneo ambamo zahanati hiyo inajegwa na hivyo kutoa fursa ya ajira na vipato kwa wananchi hao .
Uongozi wa Halmashauri kwa kushirikiana na wananchi wa chela wanaendesha zoezi hilo la usimamizi wa ujenzi wa kituo hicho na kufanya ujenzi huo kuwa na ufanisi na kwenda kwa kasi ya kutosha kwani mpaka sasa ujenzi huo umefika kwenye hatua nzuri na yakuridhisha kwani Mhandisi wa Halmashauri ya Msalala amepiga kambi katika eneo la tukio ikiwa ni kuhakikisha kuwa ujenzi huo unakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa kwani mpaka sasa imefikia kwenye hatua ya upauaji.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.