ZIARA YA KUKAGUA MAEEO YA UWEKEZAJI
Ziara ya ukaguzi wa maeneo ya uwekezaji uliofanyika katika Halmashauri ya Msalala ulibaini fulsa mbalimbali ambazo zipo ndani ya halmashauri hiyo. Baadhi ya maeneo waliyotembelea ni pamoja na Kata ya Isaka ambapo walikagua eneo lililotengwa kwaajiri ya ujenzi wa maegesho ya magari akitoa maelezo juu ya eneo hilo Afisa aridhi Ndg Mahmood Jidawy alisema eneo hilo linaukubwa ha heka 6 na tayari halmashauri ilisha walipa wananchi fidia,mbali na hayo afisa aridhi alisema kuwa eneo lipo karibu na miundo mbinu ya barabara , umeme na maji. Eneo hilo lipo hatua za mwisho kupatiawa hati milki na mpaka sasa tayari eneo hilo limekwisha tengewa kiasi cha Tsh.150,000,000 kwaajili ya uendelezwaji. Sambamba na hilo walikagua eneo la bwawa la maji lililopo kata hiyo ya Isaka na kujione shughuri nyingi za kimaendeleo zikiendelea kama vile kilimo cha umwagiliaji , uchotaji majimkwa matumizi ya nyumbani na umyweshaji wa mifugo.
Eneo linguine lililo tembelewa ni bwawa la asili lililopo katikati ya Kata ya Mwalugulu na Kata ya Isakajana katika kijiji cha Igundu bwawa hili lina ukubwa wa heka 450, eneo hilo pia linatumika kwa shughuli zingine za kibinadamu kamavile kilimo cha Viazi ,Mbogamboga mahindi na mpunga inapofika kipindi cha kiangazi. Bwawa hili liliwahi kukauka mara moja mwaka 2000 mpaka sasa bwawa hilo halijawahi kukauka .
Kata ya Bulige walikgua soko pamoja na ghara la kuhifadhia nafaka kwa wakulima lililojengwa kisasa pamoja na kuangalia eneo lililotengwa kwajili ya mladi wa ujenzi wa machinjio ya kisasa ambapo eneo hilo linaukubwa wa heka 7.
Eneo jingine lililo kaguliwa ni eneo la chanzo cha maji ya asili (chemchem ya asili )iliyopo Kata ya Chela ambapo katika chanzo hicho kunashughuli mbalimbali za kimaendeleo zinazo endelea kama vile mladi wa umwagiliaji, uchotaji maji kwa shughuli za nyumbani na unyweshaji maji mifugo.
Eneo linguine lilikuwa ni eneo lililo pandwa miembe kwa wingi eneo hilo lipo kata ya busangi ambapo mwananchi ndio wapandaji wakuu wa miti hiyo na mwaka jana matunda yaliyopatikana katika miti hiyo iliingizia halmashauri ya masala tsh 12,000,000 hivyo eneo hilo linafaa kwa uwekezaji wa kiwanda cha juisi.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.