ZOEZI LA UPIGAJI CHAPA KWA NG’OMBE LAANZA KWA MAFANIKIO MAKUBWA.
Halmashauri ya Wilaya ya Msalala yaanza utekeleaji wa upigaji chapa kwa ng’ombe ambapo zoezi limefunguliwa na Afisa Tarafa wa Kahama Mjini Ndg.Julius Ichagama kwa niyaba ya Mkuu wa Wilaya wa Kahama. Zoezi hilo lilihuzuliwa na Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala pamoja na wafuji kutoka maeneo mbalimbali. Zoezi hilo lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani wananchi na jamii ya Wafugaji iliitikia kwa kiasi kikubwa sana kwani kwa siku hiyo ya uzinduzi kwa kata ya Busangi ni zaidi ya Ng’ombe 5120 walipigwa chapa ambapo mpaka hivi sasa zoezi hilo linaendelea kwani Halmashauri ya Msalala inatarajia kupiga chapa zaidi ya ng’ombe laki moja na arobaini alfu (140,000).
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.