Kusimamia utekelezaji wa sera ya Serikali Mtandao na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Halmashauri.
Kuhakikisha vifaa vya kompyuta na mtandao wa mawasiliano vinakuwa katika hali nzuri.
Kusaidia na kutoa huduma za manunuzi ya vifaa vya kompyuta na Mtandao wa Mawasiliano katika Halmashauri.
Kuanzisha na kusimamia matumizi ya mawasiliano ya baruapepe, mtandao wa ndani na nje ya Halmashauri
Kuratibu na kusimamia uanzishwaji wa mifumo ya kompyuta na benki za takwimu katika Halmashauri
Kuratibu na kusimamia uendelezaji wa watumishi katika matumizi ya Technolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
Kufanya tafiti zinazohusiana na utumiaji wa teknolojia ya mawasiliano kama chombo cha kuimarisha utendaji, utoaji wa taarifa muhimu na huduma kwa wananchi na wadau wote.
Kutoa huduma za kitaalamu katika matumizi ya Teknolojia ya Habari kwa Halmashauri.
Kutekeleza sera ya Serikali ya mtandao (e-government)
Kuratibu utekelezaji wa usanifu na kutunza/kuiendeleza matumizi yanayohusiana na Tovuti na utunzaji wa kumbukumbu kwa ajili ya Halmashauri ya Wilaya, wizarani na wadau wengine.
Kuratibu na kutoa ushauri wa kitaalamu katika maununuzi ya vifaa vya teknolojia ya habari.