Halmashauri ya Msalala yakamilisha ujenzi wa Maabara
Katika ulimwengu wasasa watu husema ukimuelimisha mwanamke umeelimisha jamii, usemi huo ulithibitishwa na Afisa Elimu Taaluma shule za sekondari wa Halmashauri ya Msalala ndugu. Elius Nyabenda katika maadhimisho ya siku ya Elimu wilaya ni humo pale aliposema Halmashauri ya Msalala imejenga Hosteli tatu katika kata ya Chela, Lunguya na Segese ilikuwawezesha wasichana kuwakaribu na mazingira ya shule kwa lengo la kuwaepusha na vishawishi mbalimbali. Ndugu Elius Nyabenda aliongeza kwakusema Halmashauri ya Msalala imekamilisha ujenzi wa maabara katika shule 13 kati ya shule 15 nakuziwekea vifaa vyote muhimu pamoja na vyanzo vya nishati, natayari maabara zote zinatumika. ( Jumla ya maabara 13 x 3 = 39, Fizikia, chemia na Biolojia) .