Idara ya Mifugo na Uvuvi
Idara ya Mifugo na Uvuvi ni miongoni mwa Idara 13 ndani ya Halmashauri Idara hii imeundwa na sekta 2 ndogo ambazo ni:- Sekta ya Mifugo na Sekta ya Uvuvi
Mafanikio
Kutoa tiba na Chanjo za Magonjwa mbalimbali
Katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko kama vile homa ya mapafu na chambavu idara imefanikiwa kushirikisha wadau wa sekta ya mifugo katika kutoa huduma za chanjo kwa mifugo ambapo jumla ya ng’ombe 23,898 walichanjwa dhidi ya ugonjwa wa Homa ya Mapafu na ng’ombe 38,870 walichwanjwa dhidi ya ugonjwa wa Chambavu. Hii imeiwezesha Halmashauri kupunguziwa majukumu ya utoaji huduma na hivyo kuelekeza nguvu kwenye miradi mingine ya jamii kama vile elimu, Afya na Maji. Idara kupitia watalaamu wake waliopo katika Ngazi za Kata na Vijiji wameendelea kutoa huduma ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa pamoja na tiba dhidi ya magonjwa mbalimbali ya mifugo
Uboreshaji wa miundombinu ya Machinjio.
Idara imefanikiwa kuboresha miundo mbinu ya machinjio ya Kata ya Isaka kwa kuifanyia ukarabati ili iweze kukidhi vigezo na kutoa huduma bora kwa wananchi.
Kielelezo 41.Fundi wakiendelea na ukarabati wa machinjio ya Isaka
Kutoa elimu ya ufugaji bora wa samaki na utambauzi wa mifugo kwa kuweka alama.
Katika kuhakikisha elimu ya ufugaji bora wa samaki inawafikia wafugaji ili kuboresha lishe na kipato katika jamii Idara imefanikiwa kuwafikishia elimu ya ufugaji bora wa samaki wafugaji 160 katika Kata 9 za Isaka, Bulige, Kashishi, Busangi, Chela, Ntobo, Segese, Bugarama na Bulyanhulu. Kwa kupitia elimu hii, hamasa imeongezeka na wananchi wengi wameonyesha nia ya kutaka kuanza kufuga samaki. Aidha, jumla ya wafugaji 1,049 kutoka katika Kata 18 wamepatiwa Elimu juu ya umuhimu na malengo ya serikali ya kufanya ufuatiliaji, utambuzi na usajili wa mifugo kwa kupitia mikutano ya hadhara ya Wafugaji.
Kielelezo 42.Mafunzo ya ufugaji wa samaki katika Kata ya Bulige na Busangi
Idara ya Ujenzi
Idara ya ujenzi inashirikiana na idara 13 ambazo zipo ndani ya Halmashaui, idara hii imegawanyika katika sekta ndogo 3ambazo ni (i) Sekta ya Matengenezo ya Barabara, (ii) Sekta ya Majengo na (iii) Sekta ya Mitambo na Umeme.
Mafanikio
Katika kutekeleza majukumu yake, Idara iimeweza kufanikisha shughuli mbalimbali kupitia fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri na kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanaofanya shughuli za ujenzi wa majengo na matengenezo ya barabara. Wadau hao ni MIVARF, ACCACIA -BGM pamoja na fedha kutoka Serikali Kuu na kufanikisha kutekeleza mambo yafuatayo ndani ya Halmashauri ya Msalala:-
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.