KITENGO CHA UKAGUZI WA NDANI (INTERNAL AUDIT UNIT)
HISTORIA FUPI:
Kitengo cha Mkaguzi wa ndani wa Hesabu (Internal Audit Unit) kilianzishwa mwaka 2004 ikiwa ni moja ya Mkakati wa maboresho katika Usimamizi wa Fedha katika Serikali za Mitaa.
Utangulizi
Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani ni Kitengo ambacho kina jukumu la Kumshauri Afisa Masuuli (Mkurugenzi ) na kutoa ushauri kwa Idara zingine ndani ya Halmashauri ili kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Kitengo hiki kinaongozwa na Mkaguzi Mkuu wa Ndani ambaye anaripoti kwa AFISA MASUULI(Mkurugenzi ). Pia, Kitengo kinafanya kazi zake kwa mashauriano na Kamati ya Ukaguzi ya Halmashauri ya Wilaya(Audit Committee)
Madhumuni ya Kitengo
Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani kinawajibu wa kufanya kaguzi juu ya utekelezaji wa majukumu ya Halmashauri pamoja na usimamizi wa rasilimali za Halmashauri na kutoa ushauri kwa Afisa Masuuli unaolenga kuboresha huduma za Halmashauri ili kufikia Malengo yalivyopangwa.
Muundo wa Kitengo
Kitengo kinaongozwa na Mkaguzi Mkuu wa Ndani akisaidiwa na Wakaguzi wa Ndani.
Majukumu ya Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani.
Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani kina majukumu yafuatayo:-
MAJUKUMU YA KITENGO CHA UKAGUZI WA NDANI
Kutoa ushauri kwa Afisa masuuli kuhusu namna bora ya kusimamia rasilimali.
Kupitia na kutoa taarifa kuhusu namna bora ya kutumia na kuhifadhi rasilimali fedha za Halmashauri.
Kupitia na kutoa taarifa kuhusu uzingatiwaji wa kanuni na miongozo ya matumizi inayoongoza Serikali za Mitaa na Serkali kwa ujumla ili kuwa na matumizi bora ya fedha.
Kupitia na kutoa taarifa kuhusu ubora wa mifumo ya kompyuta iliyopo katika kusimamia matumizi bora ya fedha.
Kupitia na kutoa taarifa kuhusu mifumo iliyopo Halmashauri inayosimamia mali kama inakidhi mahitaji ya matumizi bora.
Kuandaa mpango mkakati wa ukaguzi.
Kuratibu shughuli za ukaguzi wa ndani.
Kufanya ukaguzi kuhusu thamani halisi ya fedha kwa huduma na bidhaa zilizonunuliwa.
Kuandaa mpango kazi wa mwaka na kuuwasilisha kwa Mkaguzi Mkuu wa ndani wa Serikali (IAGD), Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu na Kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa.
Kupitia na kutoa taarifa juu ya udhibiti wa stakabadhi na utunzaji na matumizi ya rasilimali za Halmashauri.
Kushughulikia masuala ya Ukaguzi wa Miradi (Performance Appraissal of Development Projects)
Kufanya tathmini juu ya ufanisi (Effectiveness) katika ngazi zote za Utawala kwenye Wizara/Idara/Mkoa unaohusika kuona ni jinsi gani wanasimamia mali (Resources) na kuona kama taratibu zinafuatwa.
MIKAKATI YA IDARA:
• Kuhakikisha kwamba mfumo wa udhibiti wa ndani unaimarishwa.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.