Timu ya mpira wa miguu ya wanaume ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala leo tarehe 13/09/2024 imepokelewa kwa shangwe kubwa na uongozi,
watumishi na wadau wa michezo ndani ya Halmashauri hiyo huku viongozi hao wakishindwa kujizuia kwa furaha na kuahidi kuishika mkono timu hiyo mwakani
kwani mwaka huu timu imeonyesha trela picha kamili itaonekana katika mashindano ya SHIMISEMITA 2025 hivyo nitoe tahadhari kwa timu za mpira wa miguu
za wanaume kujipanga sawa sawa kwani hatuna lelemama kwenye soka na tunautaka ushindi wa kwanza na inawezekana,hayo ni maneno yaliyosemwa na Makamu
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo MHE. Ibrahimu Six wakati wa mapokezi hayo.
Timu ya Kurugenzi Msalala imeshiriki mashindano ya SHIMISEMITA kwa mara ya kwanza mwaka huu 2024 tangu kuanzishwa kwa mashindano haya na kuibuka mshindi
wa 3 kati ya Timu 76 zilizoshiriki michuano hiyo na kupewa zawadi ya kombe la mshindi wa 3 wa mashindano hayo.Sambamba na kombe hilo mdau wa mchezo wa Kriketi
aishiye jijini mwanza alifurahishwa na namna Kurugenzi Msalala ilivyokuwa ikisakata kabumbu na akaamua kuipa seti ya vifaa vya mchezo huo ili uendelezwe ndani
ya Halmashauri ya Msalala.
Akimwakilisha Mwajiri wa Timu hiyo,Bi.Mary Nziku amemshukuru Daktari Samia Hasain Suluhu kwa kujari michezo kwani wananchi wengi wamehamasika kupitia kuona namna kiongozi mkuu wa nchi anavyoziunga mkono timu za Simba na Yanga vivyo hivyo nasi kupitia Mkurugenzi wetu Kipenzi cha wanaMsalala aliamua kugharamia ada ya ushiriki wa wanamichezo,posho za wachezaji na vifaa vya michezo ili timu hii ishiriki na kwa kweli wachezaji hamjatuangusha.Nitumie nafasi hii kumshukuru Mkurugenzi Mtendaji
wa Halmashauri ya Msalala Bi.Rose Robert Manumba kwa kuona umuhimu wa michezo kwani tangu kuanzishwa kwa Halmashauri haijawahi kutokea Timu zetu kushiriki mashindano
ya Kitaifa,nina imani mwaka ujao tutafanya vizuri zaidi.
Akiongea kwa niaba ya wachezaji wote,kocha wa Timu hiyo MWL.Kashindye ameishukuru Halmashauri kwa kuthamini michezo kwani mwaka huu tumeshiriki michezo ya pete wanawake,volleyball wanaume na wanawake,handball wanaume na wanawake na mpira wa miguu wa wanaume na ni mpira wa miguu pekee tulishinda. Wachezaji wapo wengi wazuri tatizo ni ufinyu wa bajeti kuweza kuwashirikisha wote sambamba na kuwa na kambi walau ya wiki moja kabla ya mashindano kwani wachezaji wengi wanaishi mazingira tofauti tofauti hivyo kuleta ugumu kufanya mazoezi pamoja.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.