Idara hii ndiyo kituvu kikuu cha Halmashauri, ikiwa na majukumu makubwa ya kubuni, kusimamia na kufuatilia utekelzaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa ndani ya Halmashauri. Aidha idara ya Mipango inawajibika pia katika upangaji wa Bajeti ya halmashauri kwa kila mwaka kwa kuzingatia vipaumbele vilivyowekwa sambamba na miongozo mbalimbali toka serikali kuu kupitia Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Wizara ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI.
Lengo lake ni kutoa huduma za kitaalamu katika nyanja za Mipango, Bajeti na vilevile kuratibu shughuli za Halmashauri katika kutoa uwezeshaji wa utaalamu kwa wakuu wa Idara nyingine. Seksheni hii inaongozwa na Afisa Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji wa Wilaya anayewajibika kwa Mkurugenzi Mtendaji.
Majukumu ya Idaya ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.