Idara ya Ardhi, Maliasili na Mazingira
Halmashauri ya Msalala ina ukubwa wa Km2 2,635.2 ambazo ni sawa na asilimia 5.2 (%) ya eneo lote la Mkoa wa Shinyanga. Jumla ya kaya 39,999 zenye watu 250,727 (Ke 128,498 na me 122,234) Sensa ya watu na Makazi Mwaka 2012), hivyo kufanya msongamano wa watu katika eneo la makazi kufikia watu 93.4 kwa Kilometa mraba 1.
Halmashauri ya Wilaya ya Msalala inapatikana kati ya Latitude 3015’’ na 4030’’ kusini mwa Ikweta na Longitude 31030’’ na 330000’’ Mashariki mwa Greenwich. Kaskazini inapakana na Mkoa wa Geita, Kusini inapakana na Mkoa wa Tabora, Mashariki inapakana na Wilaya ya Shinyanga na Magharibi inapakana na Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Ramani 1.Ramani ya Mkoa wa Shinyanga kuonesha Halmashauri ya Msalala
Ramani 2. Ramani ya Wilaya ya Kahama kuonesha Halmashauri ya Msalala
Katika kutekeleza majukumu yake,Idara imefanikiwa kuandaa michoro ya Makao Makuu ya Halmashauri ya Msalala katika Kata ya Ntobo pamoja kutangaza maeneo ya Ntobo, Masabi na Segese kuwa maeneo ya Mpango Mji (Planning Area).
Jumla ya michoro (5) ya mipango mji katika eneo la makao makuu Ntobo na Masabi imeandaliwa na tayari imeshapitishwa na kuidhinishwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Pia tumehuisha mchoro 1 na kuandaa mwingine 1 katika eneo la Itogwanholo, Kata ya Isaka. Michoro yote 7 ina jumla ya viwanja vya matumizi mbalimbali 4,175. Aidha Michoro yote hii imekwisha idhinishwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.(Rejea ramani 1,2,3)
Ramani 3. Ramani ya mchoro wa mipango miji eneo la Ntobo Makao Makuu.
Ramani 4.Ramani ya mchoro wa Kutangaza maeneo ya Mipango Miji.
Jedwali 3. Muhtasari wa Michoro na Idadi ya Viwanja (Makao Makuu)
NA
|
JINA LA MCHORO
|
TP NO (NAMBA YA MCHORO)
|
IDADI YA VIWANJA
|
1
|
Ntobo central area layout plan
|
TP DRG No 16/MDC/15/052016
|
575
|
2
|
Masabi neighbourhood layout I
|
TP DRG No 16/MDC/19/082016
|
737
|
3
|
Masabi neighbourhood layout II
|
TP DRG No 16/MDC/20/082016
|
823
|
4
|
Ntobo neighbouhood layout I
|
TP DRG No 16/MDC/16/072016
|
621
|
5
|
Ntobo neighbouhood layout II
|
TP DRG No 16/MDC/17/072016
|
435
|
|
Jumla
|
|
3191
|
Jedwali 4.Muhtasari wa Michoro na Idadi ya Viwanja(Maeneo mengine)
NA
|
JINA LA MCHORO
|
TP NO (NAMBA YA MCHORO)
|
IDADI YA VIWANJA
|
1
|
Itogwanholo squatter upgrading layout plan IV
|
TP DRG No 16/MDC/14/042016
|
687
|
2
|
Itogwanholo neighbourhood unit V
|
TP DRG No 16/MDC/18/082016
|
297
|
|
JUMLA
|
|
984
|
Jedwali 5. Uandaaji michoro midogo ya kina (Site-plan)
NA
|
JINA LA KATA
|
SHUGHULI
|
MATOKEO
|
1
|
KATA YA BULYANHULU
|
Kuandaa mchoro mdogo wa kina wa eneo la ujenzi wa Shule ya Msingi Kabale
|
Mchoro umekamilika na Ujenzi wa Shule hiyo umekamilika.
|
2
|
KATA YA ISAKA
|
Kuandaa mchoro mdogo wa kina wa eneo la ujenzi wa kituo cha Afya
|
Mchoro umekamilika na tayari ujenzi umeanza
|
3
|
KATA YA MWAKATA
|
Kuandaa mchoro mdogo wa kina wa eneo la ujenzi wa Sekondari ya Kata ya Mwakata
|
Mchoro umekamilika na tayari ujenzi umeanza
|
4
|
KATA YA IKINDA
|
Kuandaa mchoro mdogo wa kina wa eneo la ujenzi wa shule ya MsingiBuzima na Nyakadoni
|
Michoro imekamilika, na imekabidhiwa serikali ya kijiji tayari kwa ujenzi.
|
5
|
KATA YA LUNGUYA
|
Kuandaa mchoro mdogo wa kina wa eneo la ujenzi wa shule ya Msingi Nyangalata
|
Mchoro umekamilika, mchoro umekabidhiwa serikali ya kijiji tayari kwa ujenzi.
|
6
|
KATA YA MEGA
|
Kuandaa mchoro mdogo wa kina wa eneo la ujenzi wa shule ya Sekondari Mega
|
Mchoro umekamilika, mchoro umekabidhiwa viongozi wa kata tayari kwa ujenzi
|
Jedwali 6.Takwimu za viwanja vya zamani
NA
|
Sehemu Kilipo
|
Viwanja vilivyoidhinishwa |
Viwanja Hatua ya Demarcation |
Jumla
|
1
|
Isaka
|
582
|
-
|
582
|
2
|
Bugarama
|
336
|
-
|
336
|
3
|
Ilogi
|
627
|
-
|
627
|
4
|
Segese
|
85
|
15
|
100
|
5
|
Ntobo
|
331
|
00
|
331
|
6
|
Kakola
|
1
|
1
|
2
|
Jumla
|
1962
|
16
|
1978
|
Aidha katika kipindi cha mwaka 2016-2017 Idara imefanikiwa kupima jumla ya viwanja 414 Mchanganuo wa viwanja hivyo ni kama ifuatavyo hapa chini.
Jedwali 7.Takwimu za viwanja vipya (2016-2017)
NA
|
SEHEMU KILIPO
|
NAMBA YA USAJILI MCHORO
|
IDADI YA VIWANJA
|
1
|
Isaka
|
Plan No E21 84/35 Reg.88808
|
07
|
|
|
Plan No E21 84/36 Reg.88809
|
07
|
|
|
Plan No E21 84/37 Reg.88810
|
08
|
2
|
Segese
|
Plan No E21 196/31 Reg.88658
|
28
|
|
|
Plan No E21 196/32 Reg.88659
|
32
|
3
|
Ntobo
|
Plan No E21 196/36 Reg.20130
|
45
|
|
|
Plan No E21 196/35 Reg.20129
|
67
|
|
|
Plan No E21 196/33 Reg.88830
|
131
|
|
|
Plan No E21 196/34 Reg.88831
|
89
|
JUMLA KUU
|
414
|
Kitengo cha Usimamizi wa Ardhi.
Kitengo cha Ardhi katika Usimamizi wa Ardhi kwa mwaka 2016/2017 imefanikiwa kutekeleza majukumu yake kama ifuatavyo:
Jumla ya hati 123 zimetolewa, kwa mwaka 2016 imetoa hati 81 na kwa mwaka 2017 imetoa hati 42, pia hatimiliki 5 za kimila zimetolewa.
Jumla ya Tshs 67,043,058.23 zimekusanywa.Kwa mwaka 2016 imekusanya Tshs 22,347,686.08 na kwa mwaka 2017 imekusanya Tshs 44,695,372.15
Migogoro ya Ardhi iliyosikilizwa na kutatuliwa kipindi cha mwaka 2016/2017 ni kama ilivyo ainishwa kwenye jedwali hapa chini.
Jedwali 8.Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi maeneo mbalimbali
JINA LA MGOGORO |
AINA YA MGOGORO |
ULIVYOENDESHWA |
ULIVYOISHIA |
AGUSTINO MAFWELE NA SERIKALI YA KIJIJI CHA ISAKA STATION
|
Mgogoro wa eneo
|
|
|
MONYIWA NA KANISA LA MOROVIAN
|
Mgogoro waeneo
|
|
|
Mgogoro kati ya shule ya msingi chela na lambo la kijiji
|
Mgogorowamipaka
|
|
|
Mgogoro kati ya shule ya sekondari Bulige na wananchi
|
Mgogorowaeneo
|
Pande zote mbili zilikutana, kati ya uongozi wa shule na wananchi pamoja na wataalamu kutoka ofisi ya ardhi
|
|
Mgogoro kati ya zahanati ya segese na wananchi
|
Mgogorowa mipaka
|
Pande zote mbili zilikutana, kati ya uongozi wa zahanati ya segese, serikali ya kijiji na wananchi
|
Mgogoro umetatuliwa
|
Kitengo cha Uthamini
Kitengo cha Uthamini ni miongoni mwa vitengo vinavyounda Idara ya Ardhi na Maliasili,kitengo hiki kinashughulika na shughuli zote zinazohusiana na mambo ya uthamini. Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/2017, kitengo cha uthamini kimetekeleza mambo yafuatayo:-
Kitengo cha Maliasili
Kitengo cha maliasili kinaundwa na vitengo vidogo3 ambavyo ni kitengo cha Misitu,Nyuki na Wanyamapori.
Kitengo cha Misitu
Mafanikio
Zoezi la upandaji miti
Halmashauri inaendelea na utekelezaji wa zoezi la upandaji miti katika mwaka 2016/2017 zoezi la upandaji miti lizinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mh.Fadhili Nkulu tarehe 01/03/2017 akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala pamoja na watumishi kutoka idara mbalimbali, jumla ya miche ya miti 3,500 ilipandwa katika eneo la Makao Makuu ya Halmashauri yaliyopo Kata ya Ntobo .ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi, Halmashauri imetekeleza shughuli za upandaji miti katika kipindi cha mvua za vuli na masika katika taasisi za Serikali ikiwa ni pamoja na Shule za Msingi na Sekondari.
Mafanikio
Kielelezo 59.Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mh.Fadhili Nkulu na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala Ndg, Simon Berege wakishiriki zoezi la upandaji miti lililofanyika katika eneo zitakapojengwa Ofisi za Halmashauri ya Msalala
Ufugaji nyuki ni moja ya shughuli zinazofanywa na wananchi wa Halmashauri ya Msalala ili kujiongezea kipato.Jumla ya mizinga ya kisasa 595 na mizinga ya kienyeji 1,648 imetundikwa katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri.Uhifadhi wa mazingira ni moja kati ya faida kubwa zinazotokana na ufugaji nyuki katika maeneo ya misitu ilipotundikwa mizinga. Shughuli ya ufugaji nyuki inakabiliwa na changamoto ya uharibifu wa mazingira kutokana na shughuili za kibinadamu za uchomaji mkaa, kunipamoja na ukataji miti kwa ajili ya matimba yanayotumika kwenye migodi, ukosefu wa elimu ya ufugaji wa nyuki kitaalamu kwa kutumia mizinga ya kisasa (morden bee hive).
Kitengo cha wanyamapori kimeundwa na vitengo vidogo 3 Misitu, Nyuki na Wanyamapori.
Mafanikio
Kitengo kimeweza kuwahamasisha wamiliki wa gobore kwa kuwaandikia barua kwa kushirikiana na Maafisa Watendaji Kata zote ndani ya Halmashauri yetu kulipia ushuru wa silaha wanazomiliki kwa wakati ili kuepuka usumbufu, sambamba na hilo pia kitengo kimefanikiwa katika utoaji wa elimu juu ya taratibu za kufuata katika umiliki wa nyara za serikali zaidi elimu hiyo ililenga waganga wajadi wanaopatikana katika kata zote ndani ya halmashauri.
Kitengo kimefanikiiwa kudhibiti wanyama waharibifu zaidi ikiwa ni fisi katika kila kata walipokuwa wakijitokeza na kuvamia hivyo kusababisha vifo vya mifugo na kuhatarisha usalama wa watu waishio ndani ya kata ya hizo. Zoezi Hilo lilifanyika kwa ufanisi mkubwa kwa kushirikiana na wanakijiji wa kata husika na viongozi wao. Miongoni mwa mafanikio yaliopatikana katika shughuli hiyo ya kudhibiti wanyama waharibifu ni kama ifuatavyo:-
Ngaya ni Kata inayozungukwa na mawe makubwa ambayo inapelekea kuwa mazalia ya fisi, hivyo kutokana na uhaba wa chakula kwa wanyama hao hatarishi hupelekea kuwinda mifugo ya wakazi wa eneo hilo walioko pembezoni mwa milima hiyo na kuharibu mazao yao kama matikiti.
Katika zoezi lililofanyika siku 4 kuanzia tarehe 06/09/2016 mpaka 09/09/2016, majira ya usiku ikijumuisha Afisa Wanyamapori Msalala na Maafisa Wanyamapori wengine 2 kutoka pori la akiba la Moyowosi/Kigosi pamoja na vijana 2 (wasaidizi). Tulifanikiwa kuzunguka milima 3 kwa kutega mitego pamoja na doria za kuzunguka milima hiyo,katika zoezi hilo tulifanikiwa kuua fisi sita (6) ambao walikuwa wanahatarisha maisha ya wakazi wa eneo husika na mali zao, kwa kufuata sheria ya wanyamapori No.5 ya mwaka 2009. Pia kuna viashiria vya fisi kuwepo kwa vile bado kuna mapango ambayo ndio hasa makazi yao, hivyo baada ya zoezi hili tuliwaelekeza wananchi pindi inapotokea taarifa ya kuonekana kwa wanyama hao ifikishwe haraka ofisini kwa ajili ya kuchukuliwa hatua.
Sehemu nyingine ni Kata ya Bulyanhulu ambapo palitokea taarifa ya kuonekana fisi “spotted hyena Crocuta crocuta” ndani ya mgodi wa Bulyanhulu aliekuwa anahatarisha usalama wa wafanyakazi wa mgodi na pia kufanya shughuli za uzalishaji kusimama kwa muda. Mkuu wa Wilaya aliagiza suala hilo kushughulikiwa, hivyo kwa kushirikiana na askari wanyamapori 2 kutoka pori la Kigosi/Moyowosi mnamo tarehe 2/11/2016 mpaka 3/11/2016 aliwindwa mnyama huyo na kufanikiwa kumua majira ya saa 8 usiku na kufuata taratibu zote za sheria ya wanyamapori No.5 ya 2009 kwa ajili ya kumuhifadhi.Hivyo kuruhusu shughuli za uzalishaji kuendelea kama awali.
Kielelezo 60.Fisi alieuwawa baada ya kuvamia katika mgodi wa Bulyanhulu.
Kielelezo 61.Wanyama hatari waliopatikana wamekufa katika Kijiji cha Kakola no.9
Kata ya Chela ni miongoni mwa kata inayozungukwa na safu za mlima wa lyandilabaloha ambapo inaaminika kuwa na wanyama hatari kama fisi na mbweha wanaoweza kushambulia mifugo na watu. Hivyo kitengo cha wanyamapori kiliunda kikosi kazi kwa ajili ya kudhibiti wanyama hao hatari mnamo tarehe 28/4/2017 mpaka 30/4/2017 kuzunguka maeneo ya Chela na kufanikiwa kuua fisi (5) na mbweha (1). Hivyo kwa idadi hiyo ya wanyama hao hatari kufa kulisaidia kupunguza uvamizi kwa mifugo ya wakazi wa maeneo hayo.
Kielelezo 62 Wanyama hatarishi waliopatakana wamekufa Kata ya Chela
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.