Miradi ya Vijana na Usajili wa Vikundi
Tunatoa huduma mbalimbali za kijamii kuptia Idara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Maendeleo ya Vijana, lengo ni kuiwezesha jamii kuwa na uelewa mpana juu ya kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii katika maeneo yao sambamba na kuendesha miradi ya kiuchumi kupitia vikundi vya Wanawake, Vijana, Waviu na Yatima. Pia tunahusika na Maswala ya Ustawi wa jamii ikiwepo kusimamia haki za wanandoa na mlezi ya watoto.
Pamoja na huduma tajwa hapo juu pia tunashughulika na shughuli zifuatazo:-
SEHEMU YA VIJANA.
Sehemu ya vijana ni moja kati ya sehemu 3 zinazounda ya idara ya Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa jamii na Maendeleo ya Vijana.
Muundo wa sehemu ya vijana.
Sehemu ya Vijana imegawanyika katika sehemu ndogo tatu kulingana na muundo wa wizara kama ifuatavyo:
(i) Malezi na Makuzi.
Hii inahusika zaidi na malezi ya vijana ili kuwawezesha kuwa na afya njema. Mambo yanayohusika ni pamoja na elimu za stadi za maisha kama vile Vijana kujikinga na magonjwa kama UKIMWI, magojwa ya zinaa na ulinzi wa afya ya kijana kwa ujumla.
Aidha sehemu inalenga kuwa chachu ya kuwajengea vijana moyo wa kujitolea na kuwawezesha kushiriki katika kazi mbali za ujenzi wa taifa kwa kujitolea.
(ii) Uratibu na Uwezeshaji.
Sehemu hii inahusika na uwezeshaji wa vijana ili waweze kujikwamua katika hali duni ya maisha kwa kufundishwa mbinu mbali mbali za kujiongezea kipato. Elimu ya ujasiriamali ni jambo kubwa linalozingatiwa na pia kuwawezesha mitaji kupitia mikopo na ruzuku kutoka kwa Wahisani na Serikali.
(iii) Maendeleo ya Ujuzi.
Sehemu hii inahusika na kuwapatia Vijana elimu ya ujuzi wa aina mbali mbali ili waweze kuishi maisha ya kujitegemea. Jambo kubwa hapa ni kuwapatia mafunzo vijana. Uwezeshaji Vijana kujiunga na vyuo vya ufundi stadi, mfunzo ya uzalishaji kama vile matofali, Useremela na mafunzo mengine yanayofanana na hayo.
Utekelezaji wa majukumu ya Sehemu ya Vijana.
Sehemu ya vijana imeweza kutekelea majuku yake kwa kupitia njia mbambali kama ifutavyo:
1.KUHAMASISHA VIJANA KUJIUNGA KATIKA VIKUNDI VYA UZALISHAJI MALI.
Moja ya majukumu ya sehemu ya Vijana ni kuhamasisha Vijana katika kujiunga vikundi vya uzalishaji mali. Lengo ni kuweza kuwaweka vijana pamoja kwa lengo la kuwawezesha kwa mitaji.
Aidha lengo lingine likiwa ni kuwajenga vijana katika tabia ya kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja kwa kuimarisha ushirika. Kwa mika mitatu jumla ya vikundi kumi na sita vimeanzishwa.
2.KUTOA MAFUNZO YA UJASILIAMALI NA STADI ZA KAZI KWA VIJANA.
Wajibu wa sehemu ya vijana ni kuhakikisha kuwa vijana wanapata stadi mbali mbali za maisha ikiwa ni pamoja na elimu dhidi ua UKIMWI, madawa ya kulevya, ugonjwa wa Malaria na namna ya kupata makazi bora.
Aidha sehemu ya vijana imeweza kuendesha mafunzo ya kujikinga na UKIMWI katika kata ya Chakwale na kujumuisha vijiji vya Chakwale, Sanganjeru, Kilimani, na Madege.
Aidha sehemu ya Vijana imeweza kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa kushirikiana na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambapo jumla ya vikundi sita vilipewa mafunzo ya ufyatuaji wa matofali fungamano na ujenzi wa kutumia matofali hayo. Kwa kupitia NHC jumla ya vikundi vnne vimekabidhiwa mashine hizo kwa ajili ya kuendeleza teknolojia hii ya ujenzi wa nyumba bora kwa bei nafuu.
3.KURATIBU MBIO ZA MWENGE WA UHURU.
Sehemu ya Vijana tangu mwaka 2013 imekuwa na wajibu wa karatibu Mbio za Mwenge wa uhuru katika Wilaya, kazi ambayo imekuwa ikifanyika.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.