Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika imegawanyika katika vitengo 5 ambavyo ni Huduma za Ugani (Extension Services),Vipando (Crop ),Mboga mboga na Matunda (Horticultural crops),Lishe (Nutrition),Zana za Kilimo (Agromechanization) ,Upimaji (Land Use Survey ),Takwimu,Usimamizi na Ufuatiliaji (Statistics, Monitoring and Evaluation),Umwagiliaji (Irrigation Unit) na Ushirika (Cooperative Unit)
Mafanikio
Katika kutekeleza majukumu yake idara imeweza kufanikisha shughuli mbalimbali kupitia rasilimali za Halmashauri na pia kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanaofanya shughuli za kilimo.Wadau hawa ni pamoja na Shirika la Oxfarm, Agrics, Meru Seed, AfricaRice, Kituo cha Utafi wa Kilimo (ARI Ukiriguru), TANRICE, Musoma Food Co. Ltd, Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi na, MIVARF na hivyo kufanikiwa kukamilisha shughuli mbalimbali.
Kielelezo 30 .Ukarabati wa Nyumba ya Afisa Ugani Kata ya Ntobo
Wadau wa kilimo wakiwa katika picha ya pamoja mapema mwezi Novemba 2016 kufuatia kikao cha tathimini ya utekelezaji wa Mradi wa kuboresha teknolojia za kilimo na uongezaji wa thamani ya mazao unaofadhiliwa na Mradi wa AFRICARICE
Kielelezo 31.Wadau wa Kilimo katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mradi wa AFRICARICE
Kielelezo 32 Wadau wa zao la Mchele katika kikao cha kujadili masuala ya lishe
Kielelezo 33.Mashamba Darasa ya mazao ya Chakula na Bustani katika Kijiji cha Busindi Kata ya Bulyanhulu
Kielelezo 34.Shamba la mbegu za viazi lishe aina ya Kabodi lililopo Kata ya Isaka
Sekta ya Ushirika
Halmashauri ina jumla ya vyama vya ushirika 41 ikiwa SACCOS 11,AMCOS 12,Vyama vya Wachimbaji wadogo 10 na vingine 8 .Vyama vyote vina jumla ya wanachama 7,871.na vimekusanya Mtaji wa jumla ya Shilingi Bilioni 1.503. Kwa kipindi cha mwaka 2016/2017 Uhamasishaji na Usajili wa Vyama vipya vya Ushirika 5 umefanyika ,kati ya hivyo SACCOS 3 na vyama vingine 2 vimeandikishwa kulingana na Sheria ya Vyama vya Ushirika .Idara pia imeweza kusimamia ufungaji wa mahesabu na ukaguzi wa vyama vya ushirika ambavyo ni SACCOS 4 na AMCOS 1 na Vyama vingine 4.Vyama 22 vimesimamiwa na kufanya mikutano kupitisha makisio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2017/18 kulingana na matakwa ya kisheria na Vyama 12 kati ya hivyo vimechangia mfuko wa Usimamizi na Ukaguzi kwa viwango tofauti tofauti kulingana na mchepuo wa chama.
Mafanikio ya chama cha IBUKA MCSL
Chama cha IBUKA MCSL) Kata ya Bugarama ambacho kina wanachama 5,226 kutoka Vijiji 14 vinavyozunguka mgodi wa dhahabu Acacia Bulyanhulu .Chama kilifikia maamuzi ya kununua na kugawa mbegu za mtama tani sita (06) katika Vijiji 14 vyenye wanachama wake.
Zoezi la ugawaji wa mbegu za mtama kwa wananchi lilizinduliwa na Mbunge wa Jimbo la Msalala Mh. Ezekiel Maige ambapo kiasi cha tani 1.2 na baadae tani 4.8 ziligawiwa baadae kwa wanachi wa vijiji 14 vinavyozunguka mgodi .Kiasi cha mbegu kilichosambazwa kiligharimu jumla ya shilingi milioni 9 .Chama kimeendelea kuwa hai kwa miaka 8 na kuwa na Uongozi na Menejimenti yenye ufanisi licha ya changamoto za ukuaji kuwa nyingi. Hadi leo hii Chama kina miliki miradi, mali na rasilimali zifuatazo:-
Matrekta 03 yenye zana zote
Kumiliki Ekari 55.5 za mashamba na viwanja.
Kilimo cha Alizeti – ekari 45
Shamba la Bustani ekari 10 – Busindi
Kupeleka bidhaa ya Chakula Mgodini kupitia kampuni ya AKO Group.
Vile vile chama kimeweza
Kununua na kugawa mbegu za alizeti (tani7.8) na mtama (tani 6)
Kuwa na mali na rasilimali zenye thamani ya zaidi ya Tshs. 480.0M
Kuwa na Uongozi wa kudumu wa Chama (Bodi na Menjimenti).
Kutoa mkopo kwa IBUKA SACCOS LTD Tshs.120.0M
Kielelezo 35.Shamba la alizeti la chama cha IBUKA lililopo Kijiji cha Mwasabuka
Kielelezo 36. Vitunguu na Tikiti katika Bustani ya Chama cha IBUKA katika Kijiji cha Busindi Kata ya Bulyanhulu
Kuanza Ujenzi wa Kiwanda cha Mafuta ya Alizeti na Karanga – Ilogi, Njia Panda.
Kuvuna tikiti na vitunguu katika Bustani ya Chama- Busindi tani 18 kwa awamu 2.
Kupeleka wafanyakazi zaidi ya 286 mgodini toka vijiji vyote 14 na kuongeza manufaa kwa jamii nzima Mfano kwa Mwezi Mei 2017 mishahara ya wafanyakazi iliyolipwa kwao moja kwa moja ilikuwa Tshs. 214.m
Manufaa kwa Serikali – Mifuko ya hifadhi ya Jamii Tshs.34.4M, SDL na PAYE Tshs.26.7M, Bima ya Afya Tshs. 3.1M, Chakula Tshs. 9.5m na Mfuko wa Fidia ya kuumia kazini Tshs. 2.9M kila mwezi.
Kulipia ada wanafunzi (Shule na vyuo – Tshs.1.8m)
Msaada wa ujenzi wa ofisi na vyoo – Tshs.3.8m
Ajira kwa wafanyakazi mashambani na bustanini - Tshs.4.8m
Kufadhili timu za mpira za Bushing’we na Kakola FC Tshs. 1.5m
Kielelezo 37.Timu ya Mpira wa Miguu Kakola F.C
Utekelezaji wa Programu ya MIVARF
Katika Halmashauri ya Msalala Programu ya MIVARF inatekelzwa katika Kata 6 za Bulige,Kashishi,Ntobo,Segese,Chela na Mwanase zenye jumla ya vijiji 14 ambapo shughuli ya uongezaji wa mnyororo wa thamani wa zao la Mpunga unafanyika.Shughuli za Programu zimegawanyika katika vipengele vikuu 4 ambavyo ni:-
Uendelezaji wa Miundombinu na Mifumo ya Masoko.
Kuongeza thamani mazao (Mpunga-Msalala)
Uendelezaji wa huduma za Kifedha Vijijini.
Uratibu wa Programu.
Uendelezaji WA Miundo mbinu Na Mifumo ya Masoko
Kipengele hiki kinalenga katika kuendeleza miundombinu ya masoko ikiwemo ukarabati wa barabara, ujenzi na ukarabati wa maghala na kuzijengea uwezo Halmashauri husika katika kusimamia miundombinu hiyo kuwa endelevu.
Katika kipengele hiki Programu imekarabati Ghala 1 katika Kijiji cha Segese kwa gharama shilingi 58,920,500 pia imekarabati barabara 3, zenye jumla ya urefu wa kilometa 31 kama ifuatavyo, Chela-Nundu Km 9 kwa thamani ya shilingi. 301,750,000, Bulige-Kashishi km 9 kwa thamani ya shilingi. 259,911,500 na Kashishi-Mwamboku km 13 kwa thamani ya Shilingi. 546,415,100, Aidha Programu imejenga Soko na Ghala katika Kijiji cha Bulige kwa thamani ya Shilingi 545,955,017 ujenzi wa ghala na soko hilo umekwisha kamilika
Kielelezo 38.Jengo la Soko na Ghala la mazao ya nafaka katika Kijiji cha Bulige, Kata ya Bulige
Kuongeza Thamani Mazao
Kipengele hiki kinatilia mkazo katika utoaji wa mafunzo ya jinsi ya kuhifadhi mazao baada ya kuvunwa, Usindikaji na hifadhi ya mazao kwa Wakulima.
Kielelezo 39 Ghala ya kuhifadhia chakula wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kukagua hali ya Chakula Halmashauri ya Msalala tarehe 17/01/2017 kituo cha Isaka
Kujenga uwezo wa wakulima katika masuala ya masoko
Katika kipengele hiki Programu imejikita katika kujenga uwezo wa Wakulima kupata masoko ya uhakika ya mpunga wao kwa mkulima mmojammoja au kwa vikundi. Pia Programu imejengea uwezo Wakulima kupata taarifa mabalimbali za masoko kwa kushirikiana na Watu/Makampuni binafsi PPP (Public Private Partnership). MIVARF pia inaendeleza na kuboresha utekelezaji wa mfumo wa Stakabadhi ya Mazao ghalani (Warehouse Receipt System) ili kuongeza kipato cha wakulima. Katika Halmashauriya Msalala kuna jumla ya vikundi 41vyenye jumla ya wanachama 1,195 kati yao wanaume ni 530 na wanawake ni 665. Vikundi hivyo vilikuwa vinajengwa uwezo na mtoa huduma taasisi ya SEIDA hadi ilipofika mwisho wa mwezi Machi 2017. Vikundi hivyo kwa sasa vinasimamiwa na Idara ya Maendeleo ya Jamii kwa kusaidiana na afisa kiungo wa MIVARF na afisa ushirika.
Uendelezaji wa Huduma za Kifedha Vijijini
Katika kipengele hiki, juhudi za Mtoa huduma (SEIDA) ameweza kuwaunganisha wakulima na Taasisi ya Vision Fund ambapo kwa msimu wa 2015/2016 taasisi iliweza kukopesha wakulima jumla ya Tshs. 75,050,000/=. Idadi ya wakulima waliokopeshwa walikuwa 280 toka katika vikundi 25, na fedha hizo zilitumika kununulia pembejeo za kilimo. Kwa msimu huu 2016/2017 mikopo ya kilimo imeendelea kutolewa kwa vikundi na mpaka sasa vikundi 27 vimeshapewa mkopo wenye thamani ya shilingi milioni 110,200,000. Katika kuboresha huduma za kifedha Vijijini, Wananchi wamehamasishwa kuunda Ushirika wa Akiba na Mikopo SACCOS ambao umefanyika katika kata zote 6. Kufikia sasa Kata ya Segese wamefanikiwa kusajili SACCOs yao yenye jina la Huduma SACCOS na kata nyingine za Bulige na Kashishi zinaendelea na ukamilishaji wa usajili.
Aidha ki-ujumla Halamshauri imenufaika katika maneneo mengi kama ilivyoainishwa hapa chini:-
Ongezeko la vikundi vyenye ufahamu juu ya uongezaji wa thamani na kuunganishwa na masoko kwa zao la Mpunga katika kata sita kutoka vikundi 12 (2012/2013) hadi Vikundi 41(2016/2017)
Vikundi vyote 41 vina kamati za masoko zenye wajumbe 3 na kamati zinafahamu majukumu yao na zinafanya kazi.
Uuudwaji na usajili wa kampuni ya wakulima wa zao la Mpunga Msalala (MPAFAC) itakayosimamia uongezaji thamani zao la Mpunga mara baada ya kukamilika kwa ufadhili wa Mtoa huduma.
Kupata usaidizi (Kikundi cha Mazao) wa ununuzi wa mashine ya kukoboa Mpunga ili kuongeza thamani kutoka MIVARF yenye thamani ya shilingi. 85,500,000/=
Kupata usaidizi wa kujengewa barabara yenye urefu wa km.5 ya kuunganisha Halmashauri ya Msalala na Halmashauri ya Shinyanga Vijijni kwa thamani ya Tshs. 380,000,000/=
Usajili wa SACCOs 1 ya HUDUMA katika kata ya Segese.
Shirikisho la wakulima wa Mpunga Msalala (MPAFARC)
Halmashauri ya Wilaya ya Msalala imefanikiwa kusajili Shirikisho la Wakulima wa Mpunga ambalo ni Kampuni yenye bodi ya wadhamini. Shirikisho hili llilianza na wanachama 12 kutoka kwenye vikundi vya wakulima wa mpunga mwaka 2016. Hadi sasa Shirikisho lina jumla ya Wanachama (vikundi) 28 vyenye jumla ya wajumbe 807 .Lengo kuu la Shirikisho ni kuongeza uzalishaji, Ubora na kuongeza uhakika wa soko la mazao yao hasa Mpunga.Hadi sasa shirikisho limeendelea kusajili wanachama wapya na pia kuunda baraza la mchele litakalowaunganisha wadau wote wa sekta ya Mpunga Mafanikio hayo yamedhihirishwa na matokeo chanya kwa shuhuda za baadhi ya wanavikundi
Mafanikio ya Kikundi cha Wasindikaji wa Mpunga cha Mazao, Kahama Mjini
Kikundi cha Mazao ni kikundi cha Wasindikaji kilicho sajiliwa mwaka 2014 kikiwa na wanachama 15 wanajishughulisha na usindikaji ,ununuzi na uuzaji wa Mchele. Kikundi kupitia mradi wa MIVARF kimefanikiwa kupata mashine ya kukoboa na kupanga madaraj ya Mchele yeneye thamani ya shilingi 85,500,000 ambapo kikundi kilichangia asilimia 25 ya gharama hiyo sawa na shilingi 21,500,000.
Kielelezo 40.Wanakikundi wa kikundi cha Mazao kilichopo Mjini Kahama kimenufaika na Programu ya Mivarf kipengele cha Uongezaji thamani wa zao la Mpunga kwa Kununua Mashine ya Kukoboa Mpunga yenye uwezo wa kukoboa gunia 200 kwa siku 1.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.