TAARIFA YA SHUGHULI ZA MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII TASAF III, MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI HALMASHAURI YA WILAYA YA MSALALA
1.0. Utangulizi:
Halmashuri ya Wilaya ya Msalala ni moja kati ya Halmashauri zinazotekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (PSSN) chini ya TASAF III. Mpango huu ulizinduliwa rasmi hapa nchini mwaka 2012 na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani awamu ya nne Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, hata hivyo Halmashauri ya Wilaya ya Msalala ilizindua rasmi Mpango huu wa Kunusuru Kaya Masikini tarehe 8 mwezi wa Octoba mwaka 2014.
2.0. Utambuzi wa kaya Masikini
Baada ya uzindunzi wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini zoezi la kutambua kaya masikini lilifanyika katika vijiji 64 vya Halmashauri ya Wilaya ya Msalala kati ya vijiji 92 vinavyofanya Halmashauri ya Msalala. Vijiji lengwa katika Mpango huu ni matokeo ya utafiti uliofanywa na Kitengo cha Takwimu cha Taifa Mwaka 2002 wakati kikiendesha zoezi la kutathimini hali ya umasikini nchini. Zoezi la kuzitambua kaya masikini lilifanywa na wawezeshaji ngazi ya Wilaya kwa kushirikiana na Serikali za Vijiji husika pamoja na Mikutano Mikuu ya Vijiji.
3.0. Uhakiki na uandikishaji wa Kaya masikini
Wakati wa utambuzi wa kaya masikini zana iliyotumika ilikuwa ni dodoso ambalo mlengwa alihojiwa na taarifa zake zilichukuliwa na baadaye kuingizwa katika mfumo maalumu wa kompyuta, kunyambulishwa na baadaye majibu yalitolewa kuonesha ni kaya zipi zilikidhi vigezo vya kuitwa kaya masikini. Kaya zilizokidhi vigezo ziliingizwa kwenye zoezi la uhakiki na kuandikishwa. Katika Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Vijiji vilivyomo katika mpango huu ni sitini na nne (64) sawa na asilimia 69% ya vijiji vya Msalala. Vijiji hivi 64 vina jumla ya kaya 5813 zilizoandikishwa na zilizokuwa zinahudumiwa na Mpango huu wa Kunusuru Kaya Masikini mpaka Oktoba 2016.
Aidha lilifanyika zoezi la uhakiki wa kuondoa kaya zisizo kuwa na sifa ya kuendelea kuwa kwenye mpango, ambapo Halmashauri iliondoa kaya 153 na kubakia na kaya 5660 . Kaya hizi ziliondolewa kwa kuzingatia vigezo vya kifo,kuhama kusikojulikana, kuwa familia za viongozi na zingine kuonekana kuwa kaya zenye watu wenye uwezo. Hata hivyo zoezi la uhakiki wa kaya ni endelevu, kwa sasa Halmashauri inazo kaya masikini 5641 zinazolipwa fedha.
4.0. Uhawilishaj Fedha kwa Walengwa
Katika mwaka wa fedha 2015/2016 hadi 2017/2018 uhawilishaji wa fedha kwa kaya lengwa umeshafanyika kwa awamu kumi na nane, kwa maana kwamba kila mwaka kuwa na awamu 6. Katika kipindi chote hicho Halmashauri imepokee Tsh. 4,549,704,454.57 ikiwa ni fedha ya kaya masikini, ruzuku ya kijiji na fedha uwezeshaji na usimamizi wa malipo. Uhawilishaji fedha umefanyika kama inavyoonekana kwenye jedwali hapo chini:
Jedwali na 1 linaonesha fedha iliyolipwa kwa madirisha mawili
Na
|
MWAKA
|
MAPOKEZI YA FEDHA
|
1.
|
2015/2016
|
1,664,253,670.44 |
2.
|
2016/2017
|
1,476,120,112.13 |
3.
|
2017/2018
|
1,409,330,672.00 |
|
Jumla
|
4,549,704,454.57 |
4.10. Utoaji Elimu kwa Jamii Siku ya Malipo
Kabla ya zoezi la ulipaji fedha kwa walengwa, wawezeshaji ngazi ya wilaya hutoa mafunzo kwa walengwa, kupitia vipindi vya mafunzo kwa jamii kwa wajumbe wa kamati za usimamizi, wenyeviti wa vijiji na watendaji wa vijiji. Mafunzo yatolewayo kati vipindi hivi ni pamoja na kuwahimiza walengwa kutimiza masharti ya kukidhi vigezo vya elimu na Afya. Wawezeshaji pia uelimisha walengwa juu ya matumizi sahihi ya fedha wanazopata kama ruzuku za kunusuru kaya masikini. Kupitia mafunzo haya kuna walengwa ambao wameanzisha miradi midogo midogo ya ufugaji wa kuku, ufugaji wa mbuzi, kilimo cha bustani na hata wengine wameweza kukodisha mashamba na kununua mbegu bora na mbolea kwa ajili ya kuboresha kilimo.
4.20. Kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii
Katika halmashauri ya wilaya ya Msalala yenye jumla ya walengwa 5641 waliopo katika mpango wa kunusuru kaya masikini kwa sasa, kaya 3,731 zenye jumla ya wanufaika 22,386 zimejiunga na mfuko wa afya ya jamii katika kipindi hiki cha malipo. Idadi hii ni sawa na asilimia 66.14 ya kaya zilizoko kwenye mpango huu. Aidha kuna kaya ambazo zilizokuwa zimejiunga awali na zinaendelea kupata huduma kupitia mfuko huu. Hata hivyo zoezi la uhamasishaji wa walengwa juu ya mfuko huu unaendelea ni matarajio yetu kuhamasisha kaya zote zijiunge na mfuko huu.
4.30. Mafanikio yaliyopatikana
Jedwali linaloonesha mafanikio ya kaya masikini baada ya kupokea ruzuku kwa kipindi cha Julai 2015 hadi Machi 2018.
JUMLA KAYA
|
NG’OMBE
|
MBUZI
|
KONDOO
|
NGURUWE
|
KUKU
|
BATA
|
KILIMO
|
BIASHARA
|
NYUMBA
|
CHF
|
5641 |
252 |
1783 |
489 |
66 |
2949 |
501 |
2930 |
457 |
958 |
3731 |
Mojawapo ya mafanikio kupitia picha ni kama ifuatavyo;-
Picha 1.Baadhi ya Walengwa wakipokea fedha katika kijiji cha Kakola NA. 9.
Picha 2.Baadhi ya Walengwa waliofuga mifugo katika kijiji cha Ndala , walinunua mifugo hii kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF III).
Picha 3. Baadhi ya Walengwa waliojenga nyumba katika kijiji cha Itogwanholo , walijenga nyumba kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF III).
5.0. Changamoto
6.0. Mikakati
7.0.Hitimisho:
Ili kufanikisha adhima ya Serikali ya kupambana na umasikini kupitia Mpango huu wa Kunusuru Kaya Masikini, ushiriki wa Serikali kwa ujumla wake ni jambo la msingi. Mpango huu ni mtambuka kwani unagusa sekta nyingi za Kijamii na Kimaendeleo. Ushiriki wa Sekta za Kilimo, Afya, Elimu,Mifugo, Maendeleo ya Jamii kwa kutaja chache, ni muhimu sana katika kufanya utekelezaji wa mpango huu uweze kutoa matarajio yaliyokusudiwa. Ushiriki wa viongozi ngazi zote katika kusimamia utekelezaji wa mpango huu, ni jambo la lazima ili kufanikisha mpango huu muhimu wa kupambana na umasikini.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.