KITENGO CHA MANUNUZI NA UGAVI
Halmashauri ya (W) Msalala ina kitengo cha Manunuzi na ugavi kinachoundwa kwa mujibu wa sheria ya Manunuzi Na 7 ya mwaka 2011 kifungu na 37 na Kanuni namba 446 za mwaka 2013 ambapo sheria hiyo inaitaka taasisi ya serikali iwe na kitengo kinachosimamia usimamizi wa manunuzi (Procurement Management Unit –PMU).
Kwa Halmashauri ya (W) Msalala, Kitengo cha ugavi kina wataalamu watatu (3) ambao wanatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria ya manunuzi na kinalo jukumu kubwa la kusimamia manunuzi yote toka idara na vitengo vilivyoko kwenye Halmashauri.
MALENGO YA KITENGO CHA UGAVI NA MANUNUZI
• Kuhakikisha Sheria na Kanuni za Manunuzi zinazingatiwa.
• Kuhakikisha Huduma na Bidhaa zinapatikana kwa wakati ili Halmashauri iweze kutekeleza majukumu
mengine yanayohitjika na jamii.
• Kuhakisha bidhaa , kazi za Ujenzi na huduma zote zinalingana na thamani halisi ya Fedha
• Kuwepo na Uwazi katika Fursa mbalimbali za Zabuni.
• Kuwepo na Usawa katika kutoa Zabuni mbalimbali.
MAJUKUMU YA KITENGO CHA UGAVI NA MANUNUZI
Majukumu ya kitengo cha ugavi yameainishwa kwenye sheria ya manunuzi na 7 ya mwaka 2011 kipengele Na 38 kama yalivyo ainishwa hapa chini:-
• Kushughulikia manunuzi yote ya taasisi
• Kusaidia majukumu ya Bodi ya zabuni
• Kutekeleza maamuzi ya bodi ya zubuni
• Ni sekretarieti ya Bodi ya Zabuni
• Kuandaa na kupitia orodha ya mahitaji
• Kuandaa nyaraka za zabuni
• Kuandaa matangazo ya zabuni
• Kuandaa mikataba
• Kutoa mikataba iliyokwisha kusainiwa
• Kutunza kumbukumbu za manunuzi
• Kutunza orodha au rejesta ya kikataba yote iliyoingiwa
• Kuandaa taarifa ya mwezi ya bodi ya zabuni.
• Kuandaa mpango wa mahitaji
Aidha kitengo cha ugavi mbali na kufanya kazi na idara na vitengo vya Halmashauri, pia kinafanya kazi kwa karibu sana kwa kushirikiana na Bodi ya Zabuni ya Halmashauri ambayo majukumu yake yameainishwa na sheria ya manunuzi na 7 ya mwaka 2011 kifungu cha 33 (1) (a) –( e).
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.