Idara ya Elimu Msingi
Halmashauri ya Msalala ina Jumla ya Shule za Msingi 94, shule 91 ni shule za Serikali na Shule 3 ni za Binafsi. Idadi ya Wanafunzi ni 65,831 kati yao ke 33,414 na me ni 32,417Idara ya Elimu Msingi ina vitengo 5 ambavyo ni kitengo cha Taaluma,Elimu ya Watu Wazima,Elimu Maalumu,Vifaa na Takwimu na Utamaduni na michezo.
Mafanikio
Takwimu za mwaka 2013 hadi 2015 zinaonesha katika Halmashauri ya Msalala wanafunzi kuanzia darasa la 3 hadi la 7 walibainika kutojua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu.Wanafunzi hao walikuwa ni 1,868 kati ya 28,249 ambao ni 6%. Hata hivyo yamepatikana mafanikio makubwa kupitia mafunzo ya mara kwa mara ya walimu kazini yanayoendeshwa na Mpango wa kuinua ubora wa Elimu (Equip –Tz) yaliyochangia katika kupunguza idadi ya wasiojua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu kwa darasa la 3 hadi darasa la 7 kupungua kutoka 6% mwaka 2014 hadi 2% mwaka 2017.
Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC)
Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) ni Kitengo, kiliachoanzishwa kwa mujibu wa sheria Na.25 ya Tume ya Utumishi wa Walimu ya Mwaka 2015. Ni Mamlaka ya Ajira na Nidhamu kwa walimu walio katika Utumishi wa umma wa shule za Sekondari na Msingi Tanzania bara.
Kazi za Tume ya Utumishi wa Walimu ni kama ifuatavyo:-
Kuendeleza na kusimamia utumishi wa walimu
Kuajiri,kupandisha vyeo na kuchukua hatua za kinidhamu kwa walimu
Kuhakikisha uwiano sawa katika usambazaji wa walimu ndani ya Serikali za Mitaa na shule
Kushughulikia masuala ya rufaa za walimu zinazotokana na maamuzi ya mamlaka ya kinidhamu
Kutunza daftari na kumbukumbu za walimu
Kusimamia programu za mafunzo ya walimu kazini
Kufanya tafiti na tathmini kuhusu masuala yanayohusu utumishi wa walimu na kumshauri Mkurugenzi inavyostahiki
Kutathmini hali ya walimu na kushauri wizara yenye dhamana ya masuala ya walimu juu ya mafunzo, idadi na uhitaji wa walimu Wilaya.
Kuandaa kanuni za maadili ya utendaji kazi ya mwalimu;
Kuendeleza mfumo wa mawasiliano na ofisi za Tume ngazi ya Wilaya juu ya mambo yote au jambo lolote kuhusiana na maendeleo ya utumishi wa walimu na kuhakikisha kwamba mwajiri na Ofisi ya Tume ngazi ya Wilaya wanaendeleza kazi zao kwa mujibu wa sheria hii;
Idara ya Elimu Sekondari
Halmashauri ya Wilaya ya Msalala ina jumla ya Shule za Sekondari (15). Kati ya hizo (14) zimesajiliwa na moja (1) haijasajiliwa.Halmashauri ina Jumla ya wanafunzi 7,092 kati yao wavulana ni 3,664 na wasichana 3,428. Jumla ya walimu ni 375 Kati yao wakiume 253 na wakike 122.
Uendeshaji shule zote 15 hutegemea fedha kutoka Serikali kuu, na hutumwa shuleni kila mwezi kwa mgawanyo wa Ruzuku ya uendeshaji (Capitation Grant) na fidia ya ada ambayo ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida.Matumizi ya fedha za Uendeshaji yamegawanyika katika sehemu (5) (i)35% ni shughuli za utawala,(ii) 30% kuboresha taaluma shuleni, (iii)15% mitihani endelezi. (iv) 10% hutumika kufanya ukarabati na (v) 10% ni kwa ajili ya huduma ya kwanza hususani kwa wanafunzi wa kike.
Shughuli za ujenzi wa Maboma ya vyumba vya Madarasa, Maabara, Nyumba za walimu, Ofisi za Walimu, Mabweni, Mabwaro ya chakula pamoja na Vyoo vya wanafunzi na walimu hufanyika kwa nguvu za wananchi. Halmashauri kwa kutumia Fedha za mapato ya ndani pamoja na zinazotoka Serikali Kuu, hukamilishaji ujenzi wa majengo hayo.
Mafanikio
Idadi ya Walimu
Idadi ya Wanafunzi
Idadi ya vyumba vya madarasa Yanayohitajika, Yaliyopo na Upungufu
N.B Shule nyingi bado zina upungufu wa vyumba vya madarasa.
Mdondoko wa Wanafunzi
N.B Wanafunzi wengi huacha shule wanapoingia kidato cha 2 na 3
Idadi ya Vyumba vya Maabara
Halmashauri ya Msalala katika kutekeleza agizo la Mhehimiwa Rais wa awamu ya 4 Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete imefanikiwa kukamilisha ujenzi wa vyumba vya maabara 3(Fizikia, Kemia Na Biolojia) katika shule zote 14 zenye usajili.
Mapokezi ya fedha za ruzuku ya Uendeshaji wa elimu Bila Malipo kwa mwaka wa fedha 2015/17
Katika Mwaka wa fedha 2016/17 Kiasi cha fedha zinazopokelewa kutoka Serikali kuu kimeongezeka ukilinganisha na mwaka wa fedha 2015/16
Matokeo ya Kidato cha 4 kwa mwaka 2015 na 2016
Changamoto zilizosababisha ufaulu kushuka
Uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi.
Wanafunzi kutembea umbali mrefu kwenda shuleni na kurudi nyumbani kila siku.
Wanafunzi wengi kushugulika na kazi za kilimo na ufugaji badala ya kuweka kipaumbele katika Elimu.
Utoro wa wanafunzi.
Upungufu wa vifaa vya maabara kwa ajili ya kujifunza masomo ya sayansi kwa vitendo.
Baadhi ya walimu kufanya kazi kwa manung’uniko kutokana na kuchelewa kupandishwa vyeo na wengine kutobadilishiwa mishahara yao baada ya kupandishwa madaraja.
Mikakati ya kuinua kiwango cha ufaulu
Kushirikisha wadau mbalimbali katika ujenzi wa hosteli shuleni.
Kuhamasisha wazazi na walezi wachangie chakula cha wanafunzi.
Kushukisha viongozi wa Kata, Vijiji na vitongoji katika uhamasishaji wa mahudhurio shuleni.
Kuendelea kununua vifaa vya maabara kwa kutumia fedha za ruzuku ya uendeshaji (Capitation Grant)
Kupandisha vyeo walimu waliofikia hatua hiyo na kuwabadilishia mishahara yao kwa
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.