Wednesday 29th, January 2025
@Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala anawatangazia wananchi na wafanyakazi pia wafanyabiashara wote kuwa tarehe 07/07/2018 Waziri Mkuu Mhe. Kassimu Majaliwa atapokelewa katika mkoa wetu wa Shinyanga kwa safari za kikazi za siku 5 ambapo katika Halmashauri ya Msalala atatembelea tarehe 09/07/2018. Katika ziara hii atatembelea miradi ya soko na ghala katika kata ya Bulige, majengo ya wodi ya mama na mtoto, maabara ya kisasa, chumba cha kuhifadhia maiti na nyumba ya mtumishi vyote vipo katika kata ya Chela na atamalizia na kuona maendeleo ya ujenzi wa makao makuu ya Halmashauri ya Msalala iliyopo katika kata ya Ntobo na baadae ataongea wananchi katika kata ya Ntobo naatamaliza kwa kuongea na wafanyakazi wote katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa kahama. Wananchi tunaombwa kujitokeza kwa wingi kumpokea kiongozi wetu wa kitaifa.
Imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.