ACACIA YAIKABIDHI MABATI HALMASHAURI YA MSALALA
Mgodi wa acacia na Bulyanhulu waikabidhi Halmashauri ya Msalala jumla ya mabati 1173 ikiwa ni mwendelezo wa harakati za kupunguza uhaba wa vyumba vya madarasa kwa wanafunzi.
Makabidhiano hayo yalifanyika leo tarehe 16 Januari 2019 katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama na Kuhudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala Ndg. Simon Berege, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Kahama maafisa elimu pamoja na watumishi wengine
Akikabidhi mabati hayo Kaimu Meneja Mkuu wa Migodi ya ACCACIA na Bulyanghulu Ndg. Arthur Mgongo alisema kuwa Mabati hayo yakatumike kuezekea madarasa ili kuweza kuwajengea watoto mazingira mazuri ya kupata elimu.
Akipokea mabati hayo Mkuu wa Wilaya ya Kahama Ndg. Anamlingi Macha aliagiza kuwa zipewe vipaumbele shule ambazo tayari zimekwisha kamilisha maboma. Sambamba na hilo Ndg. Macha aliwataka wadau wengine waendelee kujitokeza ili waendelee kuchangia maendeleo ya taifa letu kwani ni haki yao ya msingi.
Jumla ya vyumba 52 vinatarajiwa kuezekwa na hivyo kupunguza upungufu wa vyumba vya madara kwa shule zetu.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.