Halmashauri ya Wilaya ya Msalala imepokea kiasi cha fedha Tsh. Milion 121 kutoka Mgodi wa Bulyanhulu ikiwa ni ushuru wa huduma. Hafra hiyo fupi imefanyika leo Tarehe 13/09/2018 katika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama na kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Ndg. annamlingi Macha , Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Msalala Dk. Ntanwa Kilagwile pamoja na waandishi wa habari.
akikabidhi Mfano wa Hundi Meneja wa Migodi ya ACACIA Ndg. Benedict Busunzu alisema kuwa lengo la kutowa fedha hizo ni kutaka kuinua hali ya kiuchumi kwa jamii na wana msalala kwa ujumla kwani fedha hizi zikielekezwa kwenye miradi ya jamii itakuwa tayali imesaidia upatikanaji wa huduma bora kwa jamii. Akipokea mfano wa Hundi hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kahama alisema kuwa fedha hizo zielekezwe kwenye miradi ya jamii kama ilivyo kawaida na si vinginevyo pia aliongeza kuwa fedha hizo zisitumike na kuishia kwenye malipo ya posho ya vikao na makongamano. Naye kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Dk. Ntanwa Kilagwile alisema kuwa fedha hizo zitaelekezwa kwenye ukamilishaji wa majengo na gharama za uendeshaji pamoja na ukarabati wa magari ya Serikali ili kuongeza tija katika utenda kazi.
Kusikiliza na kutazama nini alichokisema meneja wa ACACIA bofya link hii https://youtu.be/IzNxGusUSd8
Pia bofya hapa https://youtu.be/utBkpjKZHOU kusikiliza na kutazama ni kipi mkuu wa wilaya ya kahama alizungumza kuhusu ACACIA
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.