Baraza la Madiwani lililofanyka leo tarehe 03/04/2018, katika ukumbiwa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala na kuhudhuriwa na Kaimu katibu tawala Mkowa wa Shinyanga Ndg. Alphonce Kasonyi, Waheshimiwa Madiwani wakiongozwa na Makamo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala Ndg. Benedict Manuari, kamati ya ulinzi na usala Wilaya, Viongozi mbalimbali, Wataalam toka Halmashauri ya Msalala, pamoja na Waandishi wa Habari toka vyombo vya habari mbalimbali. Baraza hilo lilifanyika kwa umakini mkubwa ambapo Waheshimiwa Madiwani walijadili hoja za mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuiagiza Halmashauri ya Msalala kuona haja ya kuwapatia wazabuni kazi ya ukusanyaji mapato katika vyanzo vya Minada na Magulio ili kuongeza tija .
Sambamba na hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Ndg. Simon Berege alikabidhiwa Bajaji nne zenye Thamani ya Tsh. 28,000,000/=zitakazo tumika kwenye zoezi la kupambana na Kifua kikuu (TIB). Akipokea msaada huo toka kwa Katibu wa Shirika la SHDEPHA+ alilipongeza shirika hilo kwa jinsi linavyo jitowa katika kushilikiana na jamii. Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Mkurugenzi wa shirika la SHDEPHA+ Msalala amesema hiyo ni awamu ya kwanza kwani kutakuwa na mwendelezo wa utoaji wa msaada kwa jamii.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.