BARAZA LA MADIWANI LAPONGEZWA
Kikao cha Baraza la Madiwa kwa robo ya tatu kimefanyika leo tarehe 04na 05 mei, 2021 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Ntobo na Kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo kamati ya Ulinzi na Usalama ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya Ndug. Anamringi Macha.
Ambapo katika kikao hicho mkuu wa Wilaya aliwapongeza madiwani na Wataalamu kwa matumizi ya teknilojia ya kisasa katika uendeshaji wa vikao. “nawapongeza sana baraza la madiwani pamoja na wataalamu kwa kuanza kutumia vishikwambi katika kuendesha vikao(tabrets) vyenu ” pongezi hizo alizitowa jana mbele ya Baraza la madiwani mara baada ya kupatiwa nafasi ya kutowa neno
Sambamba na hilo Mkuu wa Wilaya aliipongeza Halmashaur ya Msalala kwa kufanya vizuri kitaifa katika ukusanyaji mapato ambapo aliwataka kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano .
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.