Baraza la Madiwani lililoketi tarehe 18 hadi 19 /08/2017 pamoja na mambo mengine limejadili nidhani ya watumishi na kufikia maamuzi ya kuwafuza kazi walimu 10 kwa makosa mbalimbali ikiwa ikiwa ni pamoja na kosa la utoro kazini. Na Walimu 4 kati yao walitakiwa kurudisha mishahara waliyopokea wakiwa hawapo kazini na 1 kati yao hakupatikana na hatia na hivyo kuamriwa kurudi kazini .
Akizungumza mbele ya Baraza la Madiwani na Wakuu wa Idara mbalimbali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Ndg Simon Berege alithibitisha hayo na kudai kuwa watumishi hao wamefukuzwa kazi na baadhi yao wameamriwa kurudisha mishahara yote ambayo walipokea pasipo kufanya kazi na mmoja kati yao aliamuriwa kurudi kazini baada ya kukutwa hana hatia.