Barazala madiwani la Halmashauri ya Msalala imeiomba Serikali kuipatia Halmashaurihiyo hadhi ya Wilaya kwani inakidhi mahitaji ya kuwa wilaya. Kauli hii imesemwana baraza la Halmashauri hiyo katika kikao cha robo ya nne ya kufunga mwaka2020/2021, akifafanua mwenyekiti wa kikao hicho Mhe. Mibako Mabubu amesemaHalmashauri hiyo ina kata 18 na tarafa 2 ambapo tarafa ya Isagehe ina kata zaHalmashauri ya Msalala na Halmashauli ya Manispaa ya Kahama.
Wakichangiamaoni katika hoja hii wajumbe wamesema ipo haja ya kuongeza tarafa ndani yaHalmashauri hiyo sambamba na kuitenganisha tarafa ya Isagehe ili mipaka halisiya Halmashauri hizo zionekane waziwazi na kuwezesha Serikali kutoa huduma kwawananchi wake ipasavyo. Wajumbe hao wamependekeza zizaliwe tarafa mbili, mojaiwe tarafa ya Mwalugulu ikijumuisha kata za Isaka, Mwalugulu, Jana na Mwanase.Tarafa nyingine iwe Lunguya ikijumuisha kata za Bulyanhulu, Bugarama, Ikinda,Lunguya na Shilela, kata zinazobaki zisalie Tarafa ya Msalala.
Ajendanyingine iliyoongelewa katika kikao hicho ni kupitia taarifa mbalimbali zakamati za Halmashauri ambapo kuna miradi mingi ndani ya Halmashauri inaendeleaikiwemo ujenzi wa hospitali ya Wilaya iliyopo kata ya Ntobo, ujenzi wa makaomakuu ya Halmashauri iliyopo mpakani mwa kata za Ntobo na Mega, Upanuzi wazahanati ya Isaka kuwa kituo cha Afya, ujenzi wa majengo ya shule mpya zamsingi na sekendari. Katika kikao hicho wajumbe walipendekeza Halmashaurikatika mwaka wa fedha ujao kiwekwe kipaumbele kwenye miradi viporo hasa umaliziajiwa maboma ya zahanati katika maeneo yao ili yaanze kutoa huduma, suala ambaloMkurugenzi Mtendaji (W) ndg. Andrew Fusi amekubaliana nalo na kuahidikulitekeleza.
NaeMhe. Prisca Msoma (diwani kata ya Bugarama) alihitaji ufafanuzi juu ya fedhazinazotolewa na mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu kwa wananchi ambapo Afisa MifugoDR. ntanwa Kilagwile amesema awali pesa hiyo ilitolewa kwa mtu mmoja mmojaambapo ni kinyume na matakwa ya Serikali. Kiutaratibu Halmashauri ndiyo yenyedhamana ya kukopesha vikundi hivyo akatoa rai kwa wananchi hasa vijana,wanawake na watu wenye mahitaji maalum kuchangamkia fursa hii kwani fedhanyingi za kukopa zimeshatengwa tayari kuwakopesha wananchi wote watakaokidhivigezo vya ukopaji.
Imetolewa naKitengo cha TEHAMA halmashauri ya MSALALA
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.