Bodi ya mfuko wa elimu katika halmashauri ya Msalala wilayani Kahama Mkoani Shinyanga imetoa madawati 162 kwenye shule 3 za sekondari za halmashauri hiyo ambazo zinakabiliwa na uhaba mkubwa wa madawati baada ya kupokea wanafunzi wengi mwaka huu 2018
Akikabidhi madawati hayo kwa niaba ya katibu wa bodi hiyo mweka hazina wa halmashauri hiyo Bw. Masatu Edward Mnyoro amesema kuwa madawati hayo yametolewa kwenye shule za sekondari Mwalimu Nyerere, Segese na Isaka ambapo kila shule itapata dawati 54.
Bw. Mnyoro amesema kuwa mfuko huo umeweka mkakati wa kuhakikisha wanakusanya kiasi cha shilingi milioni 200 ili kuongeza Nguvu kwa mfuko huo ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa madawati kwenye shule nyingine ambazo zinakabiliwa na uhaba wa madawati
Akipokea msaada huo wa madawati mwenyekiti wa halmashauri ya Msalala Bw, Mibako Mabubu amesema kuwa madawati hayo yataenda kwenye shule hizo na kwamba ni matumani kuwa yataenda kufanya mabadiliko kwenye shule hizo na kwamba wanafunzi wataweza kusoma bila kuwa na usumbufu kama ilivyo kuwa hapo a
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.