Ushauri huu umetolewa katika kikao cha kupitia hoja za CAG na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Tellack leo tarehe 29/06/2019 katika ukumbi wa Halmashauri ya Msalala uliopo katika kijiji cha Ntobo Kilomita 30 toka Kahama Mjini. Katika kikao hicho viongozi mbalimbali wamehudhulia wakiwepo Katibu Tawala (M) bw. Alberti Msovela, Mbunge wa jimbo la Msalala MHE. Ezekiel Maige, Mkuu wa Wilaya ya Kahama bwana Anamringi Macha, Waheshimiwa madiwani , wataalamu wa Halmashauri hiyo na baadhi ya wananchi wa Halmashauri hiyo.
Bi Zainab Tellack ameitaka Halmashauri kubuni vyanzo mbadala badala ya kutegemea ushuru wa huduma kutoka katika makampuni yanayojihusisha na dhahabu ambapo ametoa mfano wa chanzo cha mapato kuwa ni kushawishi wanunuzi wa dhahabu kuwa na masoko ndani ya Halmashauri, masoko hayo yataiwezesha Halmashauri kukusanya mapato. Mwenyekiti wa kikao hicho MHE. Mibako Mabubu ameupokea ushauri kwa niaba ya Halmashauri na kuahidi kuutekeleza.
Imetolewa na Kitengo cha TEHAMA Halmashauri ya Msalala.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.