Chf mpya ambayo inalengo la kumpunguzia wananchi mzingo wa huduma za afya kwa kujenga tabia ya kukata bima ya afya , mafunzo yake kwa watoa huduma yamefanyika leo tarehe 10/09/2018 kwa lengo la kuwawezesha watoa huduma hao kuielewa vizuri mpango mpya wa bima ya Afya ya jamii na hivyo kuwa mabalozi wazuri kwa wananchi kwani bima hii inawahusu wananchi moja kwa moja ambapo wanajamii atapaswa kujiunga kabla ya kuugua kwa kutoa Tsh. Elfu thelathini (30,000) na kukatiwa kadi za matibabu kwa watu 6 yaani mkuu wa kaya na wategemezi wengine 5 ambao watapatiwa matibabu katika zahanati zote , vituo vya afya vyote na hospitali zote za serikali ndani ya mkoa lakini mwanachama matibabu yake yanaposhindikana zahanati ni lazima mgonjwa huyo apatiwe rufaa ili aende katika ngazi nyingine ya huduma.
Akifungua mafunzo hayo kaimu mganga mkuu wa Halmashauri ya Msalala ndugu Ignance Lufulila amesema CHF ya sasa imeboreshwa Zaidi kwa kufikia mikoa yote Tanzania bara ambapo kwa sasa vituo vya kutolea huduma vitapokea malipo kulingana na wakazi waliopo katika eneo husika, wanachama hai waliojiandikisha na idadi ya wanachama hai waliopatiwa huduma katika kituo husika hivyo kuwataka watumishi wa Afya hao kuhakikisha wananchi wanahamasishwa kujiunga na bima hii sambamba na kuwahudumia vizuri wananchi ili waweze kujitengenezea fedha za kutosha kwani biashara siku zote ni matangazo kwa kutoa huduma nzuri katika vituo vyao kutachangia wananchi wengi kufika kupata matibabu hapo na hivyo kuongeza pato la kituo.
Mafunzo hayo yameendeshwa na timu ya CHF mkoa na wilaya ikishirikiana na timu ya wataalamu kutoka mradi wa tuimalishe Afya (HPSS) iliyokuwa ikiongozwa na DR. Kasale kutoka HPSS na bwana Isaack Manyonyi Afisa Tehama (M) kutoka ofisi ya Katibu tawala mkoa wa Shinyanga. Akiwasalimia washiriki Dr. Kasale amewataka watoa huduma kushirikiana na kamati za usimamizi wa vituo vyao na panapotokea tatizo au changamoto yeyote basi wawasiliane mara moja na timu ya CHF wilaya au mkoa sambamba na mdau wa mradi wa Tuimalishe Afya kwani lengo kuu ni kuhakikisha wananchi wa Tanzania anakuwa na Afya njema muda wote.
Nae mtaalamu wa mifumo ya kielektroniki ya bima ya Afya ijulikanayo kwa jina la CHF IMIS ndugu simon Gamaya amewasisitiza watoa huduma hao kuhakikisha wanachama wanaowahudumia wapo kwenye mfumo na iwapo hawatamwona kwenye mfumo amewashauri kuwasiliana na Afisa mwandikishaji kwani taarifa za mwanachama katika mfumo wa sasa huingia kwenye komputa kuu iwapo tu kila kipengele kwenye fomu ya usajili wa mwanachama utajazw kwa usahihi na kutumwa kwenye komputa kuu kazi ambayo inafanywa na Afisa mwandikishaji ambao tayari walishapatiwa mafunzo ya namna ya kusajili kwa kutumia mfumo mpya.
Kwa upande wao watoa huduma wameshukuru kwa mafunzo hayo na kuahidi kufanya kazi kwa kujitoa Zaidi ili kuwezesha wananchi kuwa na Afya bora ambazo zitapelekea taifa kusonga mbele kwa kuwa wananchi watajikita Zaidi na shughuli za uzalisha mali ambazo kutasaidia uchumi wa taifa kukua.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Halmashauri ya Msalala.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.