DIWANI ALIYESHINDA KWA KISHINDO AAPISHWA
Diwani mpya wa kata ya Bugarama Mhe. Josephat Izengo leo tarehe 30/08/2018 ameapishwa
rasmi kuwa Diwani hiyo, mhe. Izengo awali alikuwa ni diwani wa kata hiyo kupitia chama cha
demokrasia na maendeleo ( CHADEMA) na baadae kuamua kuachana na chama hicho na kujiunga
na chama Tawala ( CCM ) kwa kuwa alilidhishwa na kazi nzuri zinazofanywa na Serikali ya awamu ya
tano inayoongozwa na Mhe. Rais John Joseph Pombe Magufuli.
Diwani huyo ameapishwa katika kikao cha baraza la madiwani cha robo ya nne cha Halmashauri ya Msalala. Akimkabidhi cheti cha ushindi Msimamizi Mkuu wa uchaguzi huo Mkurugenzi wa Halmashauri
Bwana Simon Berege amemtaka Mhe. Izengo kuwatumikia wananchi wa kata ya Bugarama bila kujali
Itikadi zao za kisiasa kwani lengo la uongozi siku zote ni kuleta maendeleo kwa wananchi.
Katika kikao hicho mambo mbalimbali yalijadiliwa yakiwemo suala la upatikanaji wa maji ya uhakika
ambapo mhandisi wa maji (W) eng. Marco Chogero amesema serikali kupitia mradi wa PBR inatoa
motisha kwa miradi inayofanya kazi hivyo wananchi watunze vyanzo vya maji. Halmashauri imejipanga
kuhakikisha visima vinavyohitaji marekebisho vinakarabatiwa sambamba na kuweka pampu mpya sehemu zinazohitaji pampu hizo.
Imetolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano Halmashauri ya Msalala
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.