Kauli hii imetolewa na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kahama bwana Vicent Ndesekio wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku 16 za kupinga ukatili
kilichofanyika Kiwilaya katika Kata ya Mwalugulu kijiji cha Igunda ambapo Bwana Vicent amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Rais Samia Suluhu kwa kuleta mabilioni ya fedha ndani ya Tarafa, ametaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa kipande cha reli ya kisasa
katika kata ya isaka ambapo wananchi wengi wameajiriwa, zaidi ya Tsh.bilioni 18 zimetumika katika kukamilisha mradi wa Umeme Vijijini (REA)
katika kata za Isaka,Jana na Mwalugulu ambapo amesema katika kata ya Mwalugulu vijiji vyote wamepitiwa na Mradi huo.
Bwana Vicent amempongeza Mbunge Alhaj Idd Kassim Idd kwa jitihada zake anazozifanya za kuwaletea maendeleo wananchi wa Msalala sambamba na kuunga mkono
jitihada za Mhe.Rais Samia Suluhu kwani mwaka 2021 alipeleka chuo wasichana 60 waliopata changamoto za kutomaliza masomo yao ya sekondari na kuwalipia
ada,2022 alipeleka wasichana 50 na mwaka 2024 atapeleka wasichana 60 na kuitaka jamii kuchangamkia fursa zinazotolewa na Mbunge wao. NDG,Vicent amemshukuru
pia Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe, Mboni Mhita kwa kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama ndani ya Wilaya na kuetikia mialiko mbalimbali ndani ya Wilaya yenye
lengo la kutatua changamoto za kijamii.
Awali akimkaribisha Mgeni Rasmi,Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala ambaye pia ni diwani wa Kata ya Mwalugulu, Mhe.Frola Sagasaga amemshukuru Mhe. Rais
Samia kwa kutekeleza vema Ilani ya chama cha Mapinduzi kwani ndani ya Kata ya Mwalugulu miradi mingi imetekelezwa ikiwemo ujenzi wa kituo cha Afya Mwalugulu
ambacho kimekamilika na kinatoa huduma kwa jamii, Mradi wa Umeme Vijijini unaendelea kutekelezwa na kwa vijiji vya Igundu na Mwankima tayari unawaka japo kuna
changamoto za kiutendaji hivyo amemwomba mgeni rasmi kuwasiliana na Tanesco ili kuweza kutekeleza mradi huo kwa muda uliopangwa sambamba na kutatua changamoto
za wananchi katika vijiji vya Igundu na Mwankima.
Nae Kaimu Mkurugenzi Mtendaji(W) NDG.Judica Sumari amewashukuru wananchi wa Vijiji vya Igundu na Mwankima kwa kujitokeza kwa wingi kuhudhuria maadhimisho ya
kilele cha siku 16 za kupinga ukatili ndani ya Halmashauri ya Msalala ambapo amesema katika siku 16 wataalamu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii walitoa elimu
kwa jamii katika kata zote 18 za Halmashauri na kuongeza kusema jamii kwa kiasi kikubwa imeelimika kwani matukio ya kesi za ukatili kwa mwaka 2023 yamepungua
hivyo jamii imehamasika na ameahidi kuendeleza mapambano dhidi ya ukatili na kuwataka Watendaji wote ndani ya halmashauri kuweka ajenda ya kupinga ukatili wa
kijinsia kuwa ajenda ya kudumu katika vikao na mikutano yao yote na kuahidi kufuatilia kupitia Mihitasari ya vikao vyao.
Akisoma risala ya kilele cha maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili ndani ya Halmashauri ya Msalala, Mratibu wa kupinga ukatili kwa wanawake na watoto Bi,
Veronika Mfuko ameyataja mafanikio yaliyopatikana ndani ya Halmashauri ni kuundwa kwa kamati za kupinga ukatili wa kijinsia kwenye mikutaniko ya watu wengi
katika kata za Segese, Bulige na Bulyanhulu.Mafanikio mengine ni kufunguliwa kwa jengo shufwa(one stop center) katika kata ya Bugarama na kuanzishwa kwa huduma
ya dawati la Jinsia katika kituo cha Polisi Bugarama na watoto wa kike kujengewa uwezo wa kujiajiri kupitia mafunzo yaliyoyapata katika chuo cha ufundi stadi cha
mt.Francis kilichopo katika kata ya Mwakata.Pia ametaja ufinye wa bajeti kuwa ni kikwazo kikubwa katika utekelezaji wa shughuli za kitengo cha kupinga ukatili wa
kijinsia na kuomba changamoto hii kupatiwa ufumbuzi.
Kwa upande wao wananchi wa Vijiji vya Igundu na Mwankima wamemshukuru Mgeni rasmi kwa kuthamini mwaliko wao na kuja kusherehekea pamoja kilele cha Maadhimisho hayo
na kumwomba kutembelea vijiji hivyo mara kwa mara na kuona shughuli za wananchi hao ambao wengi wao ni wakulima wa Mpunga na kuiomba Serikali na wadau wa maendeleo
kuchangamkia fursa za uwekezaji kwa kujenga mashine za kukoboa ndani ya eneo hilo kwani kwa sasa umeme upo, hii itawasaidia kutosafirisha mazao yao kwenda Kagongwa
na hivyo kuongeza mapato kwa Halmashauri ya Msalala.Suala hili limechukuliwa na Mkurugenzi Mtendaji(W) na kuona namna ya bora ya kulifanyia kazi kwani Mkurugenzi huyo
anakutana na wadau mbalimbali nchini hivyo itakuwa rahisi kwake kufikisha taarifa hii njema kwa Taifa.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.