Kauli hii imetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Kahama ndugu Anamlingi Macha katika semina ya lishe iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala iliyopo katika kata ya Ntobo ambapo mkuu wa Wilaya huyo alikuwa mgeni rasmi wa mafunzo hayo, amewasisitiza wafanyakazi kufanya kazi kwa uzalendo pasipo kusimamiwa ili kuleta maendeleo chanya katika jamii na Taifa kwa ujumla. Jamii ielimishwe ili izingatie kutoa lishe bora kwa jamii hasa watoto walio na umri ndani ya siku 1000.
Kwa upande wao wawezeshaji wa Lishe ngazi ya kitaifa na Mkoa, wamesema tayari Wakuu wa Mikoa na Wilaya wamesaini mkataba wa kuhakikisha kila Halmashauri nchini inatoa elimu ya matumizi ya Lishe bora kwa jamii sambamba na kutumia makundi matano ya lishe bora kwani vyakula vingi vinapatikana katika maeneo yao ya halisi hivyo kinachokosekana ni elimu ya namna ya kutumia makundi hayo ya vyakula hivyo ni jukumu la kamati ya Lishe ya Halmashauri kuhakikisha jamii inaelimishwa juu ya umuhimu wa kutumia lishe bora sambamba na kuwahimiza wananchi kuandaa bustani za mboga mboga.
Katika semina hii, kamati ya lishe ya Halmashauri imepitishwa katika vipengele muhimu vya kuandaa mpango wa bajeti ya kamati ya lishe ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2019/20 na kuahidi kupanga bajeti itakayotekelezeka kwa kuweka takwimu zenye kuendana na uhalisia wa wananchi wa Msalala sambamba na kutenga Tsh. 1000 kwa kila mtoto kwa idadi yao sambamba na kuomba wadau wa maendeleo kujitokeza kusaidia kueneza elimu hii adimu kwa wananchi.
Imetolewa na kitengo cha Habari na Mawasiliano Halmashauri ya Msalala.
Haki Miliki ©2017 Halmashauri ya Msalala. Haki zote zimehifadhiwa.